Thursday, October 29, 2020

Mkongomani kumrithi Thiery Namungo

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

UONGOZI wa Namungo inatarajiwa kumleta kocha mpya raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Aidia Magloire, kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa.

Magloire anatarajiwa kuchukua mikoba ya Mrundi Thiery Hitimana ambaye amegomea kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kuifundisha Namungo

Magloire  kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya wanawake ya DR Congo na kocha msaidizi timu ya taifa ya wanaume wa nchi hiyo.

Kocha huyo ambaye ana leseni ‘A’ inayotambuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), leseni ‘A’ UEFA na mkufunzi wa CAF anatarajiwa kutua wakati wowote nchini.

Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya klabu ya Namungo, zinasema wamefikia uamuzi wa kumleta kocha huyo, baada ya  Hitimana kuwaweka ngumu.

“Kocha Hitimana tulitaka kumpa mkataba tangu Machi mwaka huu, kabla ya ligi kusimama kutokana na kuenea kwa virusi vya corona, lakini alikataa kwa kudai kuwa tusubiri hadi atakaporejea kutoka kwao Burundi,”

“Hata baada ya kurudi tukimuomba tukae mezani lakini pia alikataa kwa madai kuwa tusibiri amalize majukumu yake ya msimu huu, hili linatutia shaka kwa sababu tayari kuna timu zinaripotiwa kufanya mazungumzo nazo,”

Mtoa habari alisema kutokana na hali hiyo  wameamua kutafuta kocha mwingine atakayekuka kuchukua nafasi yake.

BINGWA lilimtafuta Mwenyekiti wa klabu ya Namungo, Hassan Zidadu, alisema kwa sasa Hitimana ni kocha wao.

“Tupo na Hitimana haitakuwa busara kumzungumzia kocha mwingine, lakini pia licha ya Hitimana kukataa kusaini mkataba na Namungo hajatuambia kwamba ataondoka, hivyo tusubiri tumalize mechi na kusikia msimamo wake ikitokea ameondoka tuweka wazi juu ya hiyo taarifa,” alisema Zidadu

Namungo wanatarajiwa kucheza na Simba Agosti 2, mwaka huu katika mchezo wa fainali wa michuano ya Azam Sports Federation Cup (ASFC), maarufu kwa Kombe FA,  utakaochezwa kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -