Wednesday, October 28, 2020

‘Mkono wa Dhahabu’ unampeleka Tambwe kwa Maradona, Messi

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA MWANDISHI WETU,

KAMA ilivyo kawaida, baada ya kumalizika kwa mtanange wa ‘Kariakoo derby’ kati ya mahasimu Simba na Yanga, lazima kutakuwa na vituko ambavyo hubaki vichwani na midomoni mwa mashabiki wa klabu hizo kongwe.

Mchezo huo, ambao ulikuwa wa kwanza kuzikutanisha timu hizo msimu huu wa soka, ulishuhudia timu hizo zikitoka sare ya bao 1-1.

Kwa lugha nyepesi, hakukuwa na mbabe, licha ya tambo za muda mrefu katika vyombo vya habari kabla ya kuanza kwa mchezo huo. Lakini licha ya sare hiyo, tambo zimeendelea kwa namna nyingine, kila timu ikitamba kwa namna yake kutokana na mambo yalivyokwenda.

Mbali na matukio mengine, bao la mshambuliaji wa Yanga, Amis Tambwe, katika mchezo wa juzi limeacha gumzo mitaani kutokana na staili aliyoitumia kuutuliza mpira kabla ya kuukwamisha kambani.

Tambwe alitumia mkono wake wa kulia kuuweka sawa mpira, kabla ya kumchambua mlinda mlango wa Simba, Vicent Agban.

Hata hivyo, Tambwe si mchezaji wa kwanza kufunga bao kwa kutumia staili hiyo, wapo waliofunga kwa mkono moja kwa moja na wengine waliutumia mkono kuweka sawa mpira na kufunga kama ambavyo alifanya Tambwe.

Tambwe anaungana na mastaa wengine duniani kuutumia mkono wa dhahabu kuipa matokeo mazuri timu yake.

Diego Maradona

Katika mchezo wa robo fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1986, akiwa na timu ya Taifa ya Argentina, Maradona aliingia kwenye historia ya ulimwengu wa soka baada ya kuunganisha kwa mkono mpira na kumzidi maarifa mlinda mlango wa timu ya England, Peter Shilton.

Haikuwa rahisi kwa mwamuzi wa mtanange huo kuliona tukio hilo, kwani Maradona aliambatanisha mkono wake na kichwa, hivyo wengi waliamini aliupiga mpira huo kwa kichwa.

Bao hilo linafahamika kama la ‘Mkono wa Mungu’ na ndilo lililoipeleka Argentina hatua ya nusu fainali.

Mpaka leo, mashabiki wengi wa Three Lions wanamchukia Maradona kwa kile alichowafanyia, kwani bao hilo liliiwezesha Argentina kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Thierry Henry

Staa huyo wa zamani wa Arsenal na Barcelona, aliwahi kutoa pasi ya mwisho kwa kutumia mkono.

Alifanya hivyo wakati timu yake ya Taifa ya Ufaransa ilipokuwa ikicheza na Jamhuri ya Ireland.

Ikumbukwe kuwa, pasi hiyo ilimfikia William Gallas, aliyepasia nyavu.

Bao hilo ndilo lililoiwezesha Ufaransa kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2010.

Katika mchezo huo wa mwisho, kama Ufaransa wangefungwa, basi wasingecheza michuano hiyo.

Baadaye, straika huyo alikiri kuwa aliunawa mpira, lakini bahati nzuri kwake ni kwamba mwamuzi Martin Hansson hakuona.

Siku mbili baadaye, baada ya kuona wachambuzi wengi wa soka wanamkosoa kwa kitendo hicho, Henry aliibuka na kudai kuwa kama staa Lionel Messi angefanya kama alivyofanya yeye, basi angeonekana mbunifu na kumwagiwa sifa kibao.

Lionel Messi

Ni mshindi mara tano wa tuzo ya Baloon d’Or na kwa kufanya hivyo, Muargentina huyo ndiye anayeongoza kwa kuichukua tuzo hiyo mara nyingi.

Katika mchezo uliozikutanisha Barcelona na Espanyol mwaka 2007, Messi alifunga bao ambalo ushahidi wa video ulionyesha kuwa mkono ulihusika.

Unajua ilikuwaje? Messi alipokea krosi kutoka kwa beki wa pembeni, Gianluca Zambrotta na ilionekana wazi kuwa alitumia mkono kuusindikiza mpira kimiani.

Bao hilo lilikuwa ni la kusawazisha lililoifanya Barca kupata sare ya mabao 2-2.

Licha ya kanda za video kuonesha kuwa Messi aliunawa mpira huo, baadaye Messi alidai kuwa hakuhisi kutumia mkono wakati alipokuwa uwanjani.

Sergio Aguero

Kwa sasa ni bonge la staa pale Manchester City na ameonekana kuwa na msaada mkubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho kinachonolewa na kocha Pep Guardiola.

Kabla ya kutua Etihad, mkali huyo alikuwa akikipiga La Liga katika Klabu ya Atletico Madrid na ndiko alikofunga bao la mkono.

Mwaka 2006, akiwa na wababe hao wa Jiji la Madrid, ambao ni wapinzani wakubwa wa Real Madrid, Aguero alipachika bao la mkono katika mchezo wa La Liga dhidi ya Recreativo.

Aguero alipokea pasi ya Mhispania Fernando Torres na ndipo alipotumia mikono yake miwili kuuweka mpira kwenye nyavu za wapinzani wao hao.

Adriano

Mbrazil huyo alitumia mkono kupachika bao katika mchezo wa Milan derby kati ya timu yake ya Inter Milan na mahasimu wao, AC Milan. Mtanange huo ulichezwa mwaka 2009, ambapo Inter waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Baada ya kupokea krosi ya Mbrazil mwenzake, Maicon, Adriano aliunganisha mpira huo uliotinga wavuni katika dakika ya 28, lakini mwamuzi hakuona tukio hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -