Sunday, November 1, 2020

MKUDE AISAIDIA YANGA KIAINA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

UNAWEZA kufikiri ni utani, lakini huu ndio ukweli wenyewe. Imebainika Jonas Mkude wa Simba ndiye aliyesaidia ubora wa kiungo wa Yanga, Said Juma Makapu ambaye kwa sasa amekuwa mchezaji muhimu mno ndani ya kikosi hicho cha Kocha Mzambia, George Lwandamina.

Makapu ameonekana kuwa lulu kwa Wanajangwani hao, baada ya Lwandamina kuonyesha kumwamini na kumwanzisha katika kikosi cha kwanza kwenye michezo ya hivi karibuni, ukiwamo dhidi ya African Lyon na Ndanda FC.

Na tangu alipojihakikishia nafasi kikosi cha kwanza, Makapu ameongeza ugumu kwa washambuliaji wa timu pinzani kuipenya safu ya ulinzi ya Yanga, huku pia akimsaidia kiungo mshambuliaji, Haruna Niyonzima, kumwezesha kupiga pasi zake hatari za mabao kutokana na kutokuwa na jukumu la kushuka kusaidia ulinzi.

Unajua ni vipi Mkude anahusika na ubora wa Makapu wa sasa? Msikie Mzanzibari huyo wa Yanga: “Sio siri, mimi mpaka kufikia hapa kupata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kunatokana na kuvutiwa na kuiga jinsi Mkude anavyocheza. Mara nyingi nimekuwa nikitaka kufanya kile anachokifanya Mkude uwanjani na hii imenisaidia sana.”

Makapu alisema mbali na kuiga vitu hivyo adimu anavyovifanya Mkude, lakini mara kadhaa amekuwa akipata ushauri kutoka kwa nyota huyo wa Simba huku akimsisitiza apambane ili kuhakikisha anapata nafasi ya kucheza.

Alisema amekuwa akiaminiwa na Lwandamina na kupewa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kutokana na kujituma mazoezini pamoja na kuiga mambo mazuri yanayofanywa na Mkude.

Katika hatua nyingine, Makapu alimzungumzia Kocha Lwandamina na kueleza kuwa alitambua uwezo wake tangu siku ya kwanza alipochukua  mikoba ya kukinoa kikosi hicho cha Jangwani akirithi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Hans van der Pluijm, aliyepewa cheo cha Ukurugenzi wa Ufundi.

“Kimsingi huyu kocha naweza kusema ni tofauti na wengine, kwanza hataki siasa lakini pia ana falsafa zake za kumwamini mtu, anaamini sana damu changa ndio maana leo utaona nacheza,” alisema Makapu.

Aliongeza kuwa Lwandamina si mtu wa mchezo mchezo, ana uwezo wa kujenga umoja ndani ya timu, lakini pia ana uwezo mkubwa wa kumhamasisha mchezaji acheze tofauti na makocha wengine.

“Ana uwezo wa kumjenga mchezaji kuwa bora, si mtu wa kukatisha tamaa pia ana uwezo wa kumfanya mtu kujiona ana deni ndani ya timu jambo kubwa zaidi hapendi kuingiliwa katika kazi yake yaani ukishindwa kucheza mpira kwake ujue umeshindwa mwenyewe na wala si majungu,” aliongeza Makapu.

Kiungo huyo aliongeza kuwa mbali na Lwandamina kumtoa mafichoni, lakini anamshukuru sana kiungo wa zamani wa timu hiyo, Mbuyu Twite, kutokana na kumhamasisha mara kwa mara juu ya kutokata tamaa.

“Niliumia sana Mbuyu alivyoondoka, ni mtu ambaye alikuwa karibu yangu sana na mara nyingi alikuwa akinipa ushauri, kunipa moyo kuwa nina uwezo wa kucheza, naona ipo siku nitacheza hatimaye nimeanza kupata nafasi sasa,” alisisitiza Makapu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -