Sunday, November 1, 2020

MKUDE AJITOSA KUMNOA FEI TOTO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

Naodha wa zamani wa Simba, Jonas Mkude, ameamua kumwongezea maujuzi kiungo wa Yanga, Feisal Salim Abdallah ‘Fei Toto’ wa Yanga, ikiwa ni siku chache baada ya wawili hao kutoana jasho katika mchezo wa watani wa jadi hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kabla ya mchezo huo, mashabiki wengi wa soka nchini walikuwa wakisubiri kwa hamu kuona iwapo Fei Toto anaweza kufurukuta mbele ya Mkude mwenye uzoefu wa aina yake.

Hatimaye baada ya dakika 90 za mchezo huo ulioishia kwa suluhu, kila aliyeshuhudia mtanange huyo alikubali kuwa Fei Toto si wa kubezwa, japo alizidiwa uzoefu na Mkude.

Mkude kwa kushirikiana na kiungo fundi wa Simba kutoka Zambia, Cletus Chama, walifanikiwa kuisambaratisha safu ya kiungo ya Yanga ambayo mbali na Fei Toto, ilimjumuisha pia Pappy Tshishimbi.

Na kutokana na kile kinachoonekana kumkubali ‘mdogo’ wake huyo, Mkude ameonekana kuwa karibu naye katika mazoezi ya timu ya Taifa, Taifa Stars, yanayoendelea kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete Park uliopo Kidongo Chekundu, Dar es Salaam.

Wawili hao ni miongoni mwa nyota wanaounda kikosi cha Stars kinachojiandaa na mchezo wa ugenini utakaopigwa Oktoba 12, mwaka huu dhidi ya Cape Verde, kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019) nchini Cameroon, mwakani.

Wakati mazoezi hayo yakiendelea, nyota hao walionekana kukimbia pamoja, huku Mkude akitumia muda mwingi kuteta hili na lile na kinda huyo wa Yanga, wakati wawili hao pamoja na wenzao wakipasha misuli moto kabla ya kuanza programu kamili ya siku.

Katika maongezi hayo, Feisal alionekana kuwa mpole akimsikiliza kwa makini Mkude ambaye anasifika kwa uwezo wake wa kumiliki dimba la chini na kutibua mipango ya timu pinzani.

Kitendo cha Mkude na Fei Toto kujifua pamoja huku wakibadilishana mawazo, kilipokewa kwa hisia kali na mashabiki waliokuwa wakifuatilia mazoezi hayo, wakiamini kiungo huyo wa Simba, alikuwa akimpa nondo mwenzake huyo wa Yanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -