Thursday, November 26, 2020

MKUDE AWAGAWA SIMBA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA EZEKIEL TENDWA

BENCHI la ufundi la Simba chini ya Kocha Mkuu, Joseph Omog, limetangaza kumvua kitambaa cha unahodha Jonas Mkude, kitendo kilicholeta mgawanyiko miongoni mwa mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi hao.

Mkude ambaye alichukua kitambaa hicho kutoka kwa Hassan Isihaka, ameenguliwa kwenye cheo chake hicho na sasa beki kisiki Method Mwanjali, ambaye awali alikuwa akitajwa kwamba atatemwa, amepewa jukumu hilo la kuwaongoza wenzake.

Mwanjali ambaye hakumaliza msimu vizuri kutokana na kupata majeraha, atasaidiwa na beki wa kushoto, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ pamoja na John Bocco aliyesajiliwa na Wekundu wa Msimbazi akitokea Azam FC.

Kutokana na kitendo hicho, baadhi ya mashabiki wa Simba wametofautiana kimtazamo wengine wakidai Mkude alitakiwa kuendelea kushikilia cheo hicho huku wengine wakidai maamuzi ya benchi la ufundi yaheshimiwe.

Juma Mgosi ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Simba alisema: “Mimi nadhani hawajamtendea haki kumwondoa kwenye unahodha, kama waliamua kufanya hivyo angalau wangemuweka kwenye unahodha msaidizi, lakini wamemwondoa moja kwa moja.”

Kauli hiyo ya Juma Mgosi iliungwa mkono na baadhi ya mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi, ambao walidai Mkude alikuwa anastahili kuendelea kuongoza kama nahodha kwani ana vigezo vyote.

Kwa upande wa wale ambao wanaunga mkono jambo hilo, wanadai kuwa mara kadhaa Mkude amekuwa na nidhamu mbovu na kwamba, Mwanjali anastahili kabisa kulibeba jukumu hilo.

“Siku zote nahodha anatakiwa awe mfano mwema kwa wenzake, sasa Mkude mara kadhaa amekuwa na nidhamu mbovu hivyo naona hakuna tatizo wakipewa wengine nafasi hiyo, Mwanjali anaonekana wazi ni kiongozi mzuri kwa wenzake,” alisema Baraka Yusuph ambaye pia aliungwa mkono na baadhi ya mashabiki wa kikosi hicho.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -