Friday, December 4, 2020

Mkutano wa kesho usigeuzwe sehemu ya kukomoana

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA MWANDISHI WETU,

MAPENZI kwa mtu au kitu ni gharama kubwa kwa anayependa. Huna ujanja kwa vile utaingia hiyo gharama.

Kesho, wanachama wa Yanga wanakwenda katika mkutano wa dharura ambao umeitishwa na uongozi wao na utafanyika kwenye makao makuu ya klabu yao katika mitaa ya Twiga na Jangwani, eneo la Kariakoo, mjini Dar es Salaam.

Tayari ajenda za mkutano huo zimeshatangazwa na uliitishwa baada ya kuanza kwa mjadala wa ukodishwaji wa klabu hiyo kwa Kampuni ya Yanga Yetu Ltd.

Mijadala imekuwa mingi, lakini inavyoendelea imekuwa ikionekana imelenga kuikwamisha Yanga, kwa kuwa baadhi ya Wanayanga hawana maelewano mazuri na mmoja wa viongozi wa juu wa klabu hiyo kutokana na masuala ya kazi au yale binafsi.

Wengi wanaozungumza wameshindwa kuweka hoja sahihi au zenye changamoto kupinga mchakato huo au kwa nini Yanga isikodishwe au kwa nini ikikodishwa itaingia matatizoni au athari ni zipi.

Wanaochangia wameonyesha wazi kutofurahishwa na jambo hilo, lakini hawachambui hoja hizo ambazo zingewasaidia wanachama kuzichambua kwa undani zaidi.

Katika mkutano ambao utafanyika kesho, Wanayanga wanapaswa kuwa na busara zaidi kuliko papara zaidi. Hawapaswi kuwa na mihemko ambayo tayari inaonekana imeanza kuikwamisha klabu hiyo katika kila mchakato.

Wenye mihemko ndio wameshindwa kutoa hoja za kuonyesha kwa nini Yanga isikodishwe. Wameshindwa kusema mambo ya msingi na wameonyesha ni chuki ambayo inawaongoza sasa kufikisha ujumbe wao.

Wanaokwenda kwenye mkutano wajichunge wasiingie katika mkumbo kama hao walioshindwa kujitafakari na kufanya mambo kwa maslahi ya Yanga na si kila mmoja kuangalia yeye kama yeye anapata nini.

Wenye jazba au wanaofanya makusudi wameshindwa kueleza Yanga ikibaki ilivyo sasa, faida yake kubwa ni ipi na ikikodishwa hasara yake kubwa itakuwaje.

Halafu wameanza kusema maneno mengi ambayo hayana uzito na zaidi kuyalazimisha, hii inaonyesha hawana hoja, lakini wanalazimisha jambo huenda kuna wanaofurahia hili litokee.

Kwa wanaokwenda kwenye mkutano wa kesho, nao watafanya hivyo, hawataweza kuonyesha utofauti wao na hao walioshindwa mapema na walifanya mambo yao kwa ajili ya Yanga.

Hakuna haja ya vurugu, hakuna haja ya kugombana na wale ambao wamepotoka na kutanguliza ubinafsi, basi wanapaswa kufundishwa kwa upendo na kuonyeshwa jambo ambalo ni sahihi.

Kufanya vurugu dhidi yao kwa lengo la kuwaumiza au kujeruhi, pia haliwezi kuwa jambo jema hata kidogo, kwani kama ni Wanayanga waliokosea, wanaweza kutengenezwa upya ili wawe msaada baadaye.

Asiyetaka kujirekebisha, atajionyesha wazi na hatafaa kuwa katika kundi moja na Wanayanga wanaotaka maendeleo kwa ajili ya klabu yao.

Asiyetaka maendeleo kwa kukataa kubadilika, basi atengwe. Kuna njia pia sahihi za kufanya hivyo bila hasira wala kuumiza. Yanga ni taasisi kubwa na ina utaratibu wake kwa mujibu wa katiba. Hivyo inaweza kushughulikia masuala yake kwa kufuata taratibu hizo bila kuumiza au kumwaga damu.

Yanga ina watu wa kila aina katika kila makundi. Si rahisi kusema hawana uwezo wa kujua uzuri na ubaya wa jambo. Yanga kukodisha timu na nembo, haliwezi kuwa jambo baya eti kwa kuwa wachache wanaotaka kumuonyesha mtu fulani.

Pia si lazima jambo lifanyike Ulaya kwanza, halafu ndiyo lifanyike Tanzania. Kushangaa ukodishaji bila kuzungumzia faida au hasara zake, ni jambo jingine la upotezaji wa muda na kuchelewesha maendeleo.

Tuwatakie Yanga kila la heri kesho, wafanye mkutano wenye amani na mwisho uwe na matunda badala ya madhara.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -