Thursday, October 22, 2020

Mkutano Yanga uko pale pale

Must Read

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

NA SALMA MPELI

MKUTANO Mkuu wa dharura wa klabu ya Yanga uko pale pale na maandalizi kuelekea kwenye mkutano huo utakaofanyika Oktoba 23 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kaunda yanaendelea vizuri, anasema Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Baraka Deusdedit.

Baraka aliliambia BINGWA jana kuwa kwa sasa wanaendelea na maandalizi huku wakiamini kuwa wanachama wamepata muda wa kutosha kupitia Ajenda za mkutano huo unaotarajiwa kuandika historia mpya kwenye klabu hiyo ya Jangwani.

“Maandalizi ni mazuri na kila kitu kinakwenda sawa, wanachama wanajiandaa na mkutano na wanachosubiri sasa ni muda tu ufike ufanyike huu mkutano ili hili suala liishe,” alisema Baraka.

Yanga imepanga kuitisha mkutano huo mkuu wa dharura kwa ajili ya kupitia mkataba baina ya klabu hiyo na Kampuni ya Yanga Yetu Limited waliouingia mwezi uliopita kwa ajili ya kuikodisha timu hiyo.

Katika hatua nyingine, wakati maandalizi hayo yakiendelea vizuri, Baraza la Wazee la Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Mzee Ibrahim Akilimali, jana lilifanya mkutano na waandishi wa habari na kuendeleza msimamo wao wa kupinga kukodishwa kwa klabu hiyo.

Akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, Mzee Akilimali alisema suala la kuiingiza timu yake kwenye kampuni na kukodishwa linaweza kusababisha madhara na kuigawa klabu yao kwenye makundi makundi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Wanaompenda Carlinhos wapewa dili

NA ASHA KIGUNDULA      MASHABIKI na wanachama wa Yanga, wakiwamo wale wanaovutiwa mno na uchezaji...

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote tatu katika mechi za Ligi...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -