Tuesday, October 20, 2020

MKWABI KUING’ARISHA SIMBA AFRIKA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA HUSSEIN OMAR


KUMEKUCHA Simba, mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa klabu hiyo uliopangwa kufanyika Novemba 4, mwaka huu, Swedi Mkwabi, alizindua kampeni yake jana jijini Dar es Salaam na kueleza mikakati yake mbalimbali ya kuiletea maendeleo timu hiyo.

Kipenga cha kampeni za uchaguzi huo ambao utakuwa wa kihistoria tangu timu hiyo ianzishwe mwaka 1936, kimeshapulizwa tangu Ijumaa iliyopita na sasa kilichobakia ni wagombea kunadi sera zao.

Akizungumza na BINGWA jana, Mkwabi ambaye aliwahi kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano kwa nyakati tofauti, alisema endapo atapewa nafasi ya kuongoza atahakikisha Simba inatisha Afrika.

“Uwezo wa kuongoza mpira ninao kwa kutumia elimu yangu ya stashahada ya juu ya Biashara na Utawala, nitaifanya Simba kutisha na kuwa kama TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,” alisema Mkwabi.

Mkwabi pia alisema kwa kutumia weledi na uzoefu wake katika soka kwa kushirikiana na viongozi wenzake, pamoja na Mwekezaji Mkuu wa klabu hiyo, Mohamed Dewji  ‘Mo’, atapambana kadiri ya uwezo wake kuziondoa changamoto mbalimbali zilizopo na kutengeneza utaratibu bora wa kuzitatua kulingana na mahitaji ya sasa ya katiba mpya ya timu hiyo.

“Nikiweza kuchaguliwa na kupata nafasi ya kuwa mjumbe wa bodi ya wakurugenzi wa Simba Sports Club Company Limited, nitatatua changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikiigharimu timu yetu,’’ alisisitiza Mkwabi.

Alieleza atahahakikisha anasimamia vizuri mfumo wa mabadiliko wa uendeshaji wa klabu ya Simba, kulingana na katiba mpya toleo la mwaka 2018 kama ilivyopitishwa na wanachama.

Mkwabi ni mgombea pekee katika nafasi ya urais, baada ya Mtemi Ramadhan kujitoa dakika za mwisho katika kinyang’anyiro hicho.

Wajumbe waliochukua fomu ni Hussein Mlinga, Idd Kajuna, Ally Kaduguda, Mohamed Seleman Said, Abdallah Mgomba, Christopher Mwansasu, Alfred Elia, Mwinda Kaduguda, Ally Suru, Said Tully, Juma Pinto, Hamis Mkoma, Abubakari Zebo, Omary Mazola, Patrick Rweyemamu na Seleman Omary Seleman.

Kwa upande wa wanawake waliojitosa kuwania ujumbe ni Asha Baraka na Jasmine Badar Soudy.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -