Thursday, October 22, 2020

MKWANJA

Must Read

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

MANCHESTER, England


 

WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, amewapa mtihani mzito mabosi wa timu hiyo, akiwaambia hataanguka saini katika mkataba wanaotaka kumpa endapo hataongezewa mshahara.

Anachokitaka nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani ni ongezekano la pauni 100,000 (zaidi ya Sh mil 290 za Tanzania) katika mshahara anaopokea sasa pale Etihad.

Sterling analipwa pauni 175,000 (zaidi ya Sh mil 520), hivyo kama uongozi wa Man City unataka kumwona akiendelea kuvaa uzi wa timu yao, basi waandae jumla ya pauni 275,000 (zaidi ya Sh mil 819) kwa wiki.

Bado kuna mazungumzo kati ya pande hizo mbili, kwa maana ya wawakilishi wa Man City na mabosi wa Man City na imeripotiwa kuwa Sterling anataka kubaki Etihad.

Endapo uamuzi wa mabingwa hao watetezi wa taji la Ligi Kuu msimu huu watakubali, basi Sterling atakuwa amempiku kwa mshahara straika wa Manchester United, Romelu Lukaku.

Kwa mkwanja huo, Mwingereza huyo atatinga moja kwa moja ‘top six’ ya mastaa wanaolipwa mkwanja mrefu Ligi Kuu ya England (EPL), baada ya Kelvin De Bruyne, Paul Pogba, Mesut Ozil na Alexis Sanchez.

Sanchez anayeongoza orodha hiyo anapokea pauni 350,000 kwa wiki pale Man United, Harry Kane wa Tottenham na Mesut Ozil, wanafuata wakiwa wanalipwa pauni 300,000 kila mmoja.

Mchezaji wa bei ghali katika historia ya Man United, Paul Pogba, ndiye anayeifunga ‘top three’ kwa kuwa kila wiki akaunti yake ya benki huingiziwa pauni 290,000 na mabosi wa timu hiyo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

UKITELEZA KWISHNEI

NA ASHA KIGUNDULAMIAMBA ya soka nchini, Simba na Yanga, leo wana vibarua vigumu vya kusaka pointi zote...

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na Staa Wako, safu inayokupa nafasi...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -