Sunday, January 17, 2021

MKWASA: WANATAKA KUTUTOA KWENYE RELI

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

bony

NA ZAITUNI KIBWANA

SIKU moja baada ya Kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment kutangaza kulipiga mnada jengo la Yanga, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Charles Mkwasa, amedai sakata hilo limelenga ‘kuwatoa kwenye reli’ kuelekea mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Agosti 23, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kampuni hiyo ilitangaza kulipiga mnada jengo hilo kesho kutokana na deni la kodi ya ardhi na malimbikizo ya Sh milioni 360 tangu mwaka 1996 hadi sasa.

Akizungumzia sakata hilo, Mkwasa alikiri klabu yao kudaiwa na Wizara ya Ardhi na Nyumba na kwamba wapo katika mpango wa kulilipa.

Alisema kuwa, waliandika barua kwenda Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Ilala kuomba kuanza kulipa fedha hizo mara Ligi Kuu Tanzania Bara itakapoanza, kwa kuwa hawana chanzo kingine cha mapato.

“Sisi hatuna chanzo chochote cha mapato zaidi ya mapato ya mlangoni, tumeandika barua kuwaomba tuwe tunawapa asilimia 25 ya mapato hayo ligi itakapoanza,” alisema.

Alisema kuwa, pamoja na hilo, pia wameomba kupunguziwa fedha hizo kwa kuwa wanalipa fedha nyingi ambazo hazilingana na thamani halisi ya ukubwa wa eneo lao.

“Tumeomba tupunguziwe, ukiangalia hili deni ni la toka mwaka 1996, halafu kila mwezi tunapaswa kulipa Sh milioni 16, ni nyingi mno, tumeomba tupunguziwe,” alisema.

Mkwasa, ambaye ana rekodi nzuri ndani ya klabu hiyo kuanzia akiwa mchezaji hadi kocha wa Yanga, alisema kuwa wanafanya jitihada kuhakikisha wanaanza kulipa deni hilo haraka iwezekanavyo.

“Sisi tunafanya jitihada, kuna hatua tulizopitia, ila wenzetu wa Msolopa wanaonekana kutuharakisha kwa kuwa wao wana asilimia 10 yao,” aliongeza Mkwasa.

Alisema kuwa leo anatarajiwa kuambatana na Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, kukutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, kujadiliana kuhusu suala hilo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -