Tuesday, January 19, 2021

Mmoja wao atamrithi ‘Big Sam’ England

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

LONDON, England

WIKI kadhaa zilizopita, Chama cha Soka cha England (FA) kilitangaza rasmi kuachana na mkufunzi, Sam Allardyce, kwa madai kuwa kocha huyo alijihusisha na vitendo vya rushwa.

Hivi sasa, benchi la timu ya Taifa ya England linaongozwa na Gareth Southgate ambaye alikuwa akikinoa kikosi cha vijana wenye umri chini ya miaka 21.

Allardyce ameachana na Three Lions baada ya kuiongoza kwa siku 67 pekee huku akiwa amecheza mchezo mmoja pekee wa kimataifa.

Ikizingatiwa kibarua cha Southgate ni kwa kipindi kifupi tu, wafuatao ni makocha wanaoweza kupewa mikoba ya kuinoa England.

Gary Neville

Neville ndiye aliyekuwa msaidizi wa Roy Hodgson ambaye alitangaza kung’atuka baada ya kumalizika kwa Fainali za Mataifa ya Ulaya za mwaka huu ‘Euro 2016’ zilizochezwa nchini Ufaransa. Hodgson alipoachia ngazi, Neville alikuwa akipewa nafasi kubwa ya kukalia kiti chake.

Wakosoaji wameibuka na kudai kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United hafai kuinoa England kutokana na matokeo mabovu aliyoyapata akiwa na Valencia.

Wameongeza kuwa alikuwa kwenye benchi la ufundi wakati England ilipovurunda Euro 2016, hivyo hana ‘CV’ za kueleweka.

Gareth Southgate

Ni rafiki mkubwa wa viongozi wa FA na hilo lilisababisha apewe kazi ya kukinoa kikosi cha vijana wenye umri wa chini ya miaka 21.

Aliwahi kukiri kutamani nafasi hiyo ya kuinoa Three Lions, ingawa hivi karibuni amedai kuwa hayuko tayari.

Wachambuzi wa soka wanaamini kuwa Southgate hana uzoefu wa kutosha wa kupewa mtihani huo mzito.

Wamekumbusha kuwa staa huyo wa zamani wa England ameshindwa mara mbili kukiongoza kikosi cha vijana kushiriki michuano ya Euro.

Alan Pardew

Wengi wanaomtaja kuwa miongoni mwa makocha wenye jina kubwa England kutokana na uzoefu alionao katika ulimwengu wa soka.

Kama alivyosema Southgate, Pardew naye aliwahi kudai kuwa huu si wakati mwafaka kwake kukabidhiwa benchi la ufundi la Three Lions.

Lakini hivi karibuni ameibuka na kauli kuwa angetamani siku moja kufundisha soka katika ngazi ya taifa.

Hata hivyo, Pardew hana rekodi nzuri katika klabu kadhaa alizowahi kufundisha ambapo aliishia kutimuliwa.

Kutokana na mwenendo usioridhisha, mabosi wa Newcastle walimfungulia mlango wa kutokea na amewahi kukutwa na hali hiyo alipokuwa akiinoa West Ham.

Steve Bruce

Ni rahisi kwa FA kumpata Bruce kwa sababu hana timu baada ya kufukuzwa na uongozi wa Hull mwezi uliopita.

Kabla ya Allardyce kupewa ‘shavu’, Bruce alikuwa na nafasi kubwa ya kuliongoza benchi la ufundi la Three Lions.

Bruce alitimuliwa Hull mara baada ya kuingia kwenye vita ya maneno na wamiliki wa klabu hiyo.

Jurgen Klinsmann

Kwa sasa, Klinsmann anakinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Marekani. Katika orodha hii ya makocha, Mjerumani huyo ndiye anayeonekana kuwa na uzoefu mkubwa wa mashindano ya kimataifa.

Kabla ya kutua Marekani, kocha huyo mwenye umri wa miaka 52 aliiongoza Ujerumani kwa takribani miaka mitatu.

Eddie Howe

Howe amejijengea umaarufu mkubwa Ligi Kuu England kutokana na soka la uhakika la timu yake ya Bournemouth.

Ndiye aliyeipandisha daraja timu hiyo kabla ya kuifanya kuwa moja kati ya timu tishio kwa vigogo.

Akiwa na umri wa miaka 38, atakuwa kocha wa kwanza mwenye umri mdogo kuifundisha Three Lions.

Wiki mbili zilizopita, Howe aliwaambia waandishi wa habari kuwa hatasita ikiwa atafuatwa na FA kuchukua nafasi ya Allardyce.

Arsene Wenger

Hivi karibuni, Mfaransa huyo alisherehekea kutimiza miaka 20 tangu alipopewa kazi ya kuionoa Arsenal.

Kwa msingi huo, Wenger ana uzoefu mkubwa na soka la England na hilo linampa sifa ya kuifundisha Three Lions.

Mara kadhaa, Wenger amekuwa akipuuzia kujiunga na benchi la ufundi la England, lakini hivi karibuni ameonekana kuvutiwa na mpango huo ingawa mkataba wake na arsenal utamalizika Juni mwakani.

Louis van Gaal

Unashangaa nini? Ndiyo, Van Gaal anaweza kupewa mikoba ya kukinoa kikosi cha England.

Licha ya kufanya vibaya akiwa na Manchester United, bado ukongwe wake katika soka la kimataifa unaweza kuisaidia Three Lions.

Alivurunda msimu uliopita pale Manchester, lakini hakuna ubishi kuwa Van Gaal ni mmoja kati ya makocha wenye mafanikio makubwa wakiwa na timu za taifa.

Alikuwa kiongozi wa benchi la ufundi wakati Uholanzi ilipofika hatua ya nusu fainali ya michuano ya  Kombe la Dunia ya mwaka 2014.

Ni rahisi kwa FA kumpata kocha huyo wa zamani wa Barcelona na Bayern Munich kwani hana kazi tangu alipotimuliwa Old Trafford miezi kadhaa iliyopita.

Faida kubwa ya Van Gaal ni kwamba, si mgeni wa soka la England na anawajua wachezaji wengi wa kikosi hicho, hivyo ni rahisi kufanya nao kazi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -