Thursday, December 3, 2020

MNATAKA WENGER AONDOKE! NANI ANA UWEZO WA KUBEBA MIKOBA YAKE?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

MJADALA mkubwa umeibuka wakati wa kipindi cha televisheni ya Sky Sports kiitwacho ‘Sunday Supplement’ juu ya nani ana uwezo wa kubeba mikoba ya Arsene Wenger kama kocha huyo ataondoka Arsenal kama baadhi ya mashabiki wa Gunners wanavyotamani.

Tayari kuna orodha kubwa ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi ya Wenger kama akina Carlo Ancelotti na Marco Silva, lakini wataweza kufuata njia za kocha huyo aliyeiweka Arsenal juu miaka yote?

Wenger atamaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu na tayari amekwishatangaza kwamba hatima yake itajulikana Machi au Aprili.

Pia imedaiwa kwamba mkataba wa miaka miwili uko mezani kwake, huku akiongeza kwamba ana mpango wa kuendelea kufundisha soka kwa miaka mingine minne.

Kama ataondoka mwishoni mwa msimu, mchambuzi wa Daily Mirror, John Cross, anafikiri kwamba Arsenal watahitaji mtu wa kuziba pengo lake mwenye uwezo na heshima kama Wenger.

“Nafikiri unapaswa kumwangalia (Thomas) Tuchel pale Dortmund na Max Allegri kule Juventus, nani unafikiri anataka kazi hiyo? Ingawa bado Wenger anataka kuendelea,” alisema Cross.

“Kuna makocha wengi wanaoweza kuitaka kazi hiyo. Nafikiri (Diego) Simeone atavutiwa, kama hataweza kufanya vizuri hilo ndilo suala la kujiuliza na sifikirii kama atamudu, kwakuwa watamtaka mtu ambaye ni mkimya na atacheza soka zuri, kama Wenger kwa miaka 20. Wataweza kucheza staili ya kupiga pasi na kushambulia.

“Roger Schmidt kutoka Bayer Leverkusen labda anaweza. Binafsi nafikiri unahitaji mtu mwenye msimamo. Pia nafikiri wanahitaji mtu mwenye uwezo wa kumwambia mtu kama (Mesut) Ozil kwamba nataka kuiinua hii klabu kwenye kiwango kingine, hivyo nataka ubaki.”

Mchambuzi wa Telegraph, Jason Burt, anafikiri kwamba kuna makocha wengi wanaoweza kufanya kazi Arsenal kama Wenger, ambaye alianza kufanya kibarua hicho tangu mwaka 1996, hadi sasa.

“Ni moja ya kazi ngumu kuitafutia mbadala wake Ligi Kuu England,” alisema Burt. “Lakini kila kitu kina mbadala wake. Una uwanja, uwanja wa mazoezi, bajeti nzuri, fedha, mashabiki, una kila kitu. Hivyo kufuata nyayo za Wenger sidhani kama itakuwa ngumu kama ilivyokuwa kwa (Sir Alex) Ferguson. Nafikiri kuna tofauti hapo.

Ancelotti hajakuwa na mambo mazuri ndani ya Bayern Munich na najua ukweli kwamba anaipenda klabu ya Arsenal.

“Alipoondoka Chelsea alirejea Arsenal kimya kimya kuangalia mambo yanavyokwenda. Atavutiwa sana na kazi hiyo.

Pamoja na Burt kusema kuna uwezekano wa kuziba pengo la Wenger, lakini alionyesha kuwa na shaka akisema: “Nafikiri kunahitajika kufanya marekebisho kidogo na si kupata mbadala zaidi, bali ikiwezekana apatikane kocha chipukizi afanye kazi na mtu mwingine pembeni yake kama mkurugenzi wa soka.

“Hayo ni mabadiliko ambayo yanaweza kufanyika, lakini kunaweza kukawa na makocha wengi wa kuziba nafasi hiyo. Hili ni suala ambalo linatakiwa kufanyika kwa sasa na nafikiri litasaidia kama Wenger akiamua kusema naondoka mwisho wa msimu huu.

“Watu wanaweza kusema yote yametokea kutokana na matokeo ya Bayern, ni kweli? Si kweli kwamba matokeo ya mechi moja yasababishe hayo. Maamuzi ya kuweka kocha mpya na mkurugenzi wa soka itasaidia klabu na kuifanya klabu isonge mbele.”

Naye mchambuzi wa Sunday People, Steve Bates, amesema Arsenal wamechelewa kupanda basi kwa kushindwa kumnasa Pep Guardiola alipoondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu uliopita.

Pia alisema walipoteza nafasi ya kumnasa Marco Silva, ambaye kwa muda mfupi aliotua Hull City amefanya vizuri na kuibadilisha timu hiyo ikicheza soka la kuvutia.

“Anafanya kazi nzuri. Kama unakuwa na kocha mwenye uwezo na kufanya kazi na mtu mwingine, itakuwa vizuri sana,” alisema. “Lakini haiwezi kutokea kiurahisi.”

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -