Wednesday, October 21, 2020

MO abebeshwa jukumu zito Msimbazi

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA MWANDISHI WETU

SIMBA inataka kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu. Hili liko wazi na ndiyo maana, uongozi wa klabu hiyo umekuwa na mikakati mbalimbali, mojawapo ikiwa ni mkakati wa kumkabidhi timu Mohammed Dewji ‘MO’, si kwa ajili ya umiliki tena, bali ni kwa ajili ya kuwa mdhamini mkuu.

Simba inaendelea kupata neema baada ya mwanachama huyo kumaliza tatizo Simba kwa kuwalipa mishahara pamoja na kutoa fedha za usajili wa baadhi ya wachezaji,  ikiwemo waliokuwa wametajwa kumaliza mikataba yao.

Wachezaji wanaotarajia kumaliza mikataba yao ni Jonas Mkude, Said Ndemla na wengine waliokuwepo katika mipango ya kocha mkuu wao, Joseph Omog.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Simba

zilieleza kwamba, baada ya kukaa pande zote mbili walikubaliana kwanza aingie kama mdhamini mkuu wa klabu wakati mchakato wa kufanya mabadiliko  ya mfumo wa uendeshaji wa klabu hiyo kwa mfumo wa kuuza hisa ukiendelea kwa utaratibu uliowekwa na Serikali.

Mtoa habari huyo alisema kabla ya kutangaza rasmi MO kuingia mkataba wa udhamini,  uongozi utaitisha kikao kwa ajili ya kufanya mabadiliko na kuboresha katiba yao.

“Unajua hivyo vyote anavyotoa MO havipo katika mchakato huo wa hisa, bali ni ahadi yake aliyotoa kwa Wanasimba kama mwanachama, licha ya kulipa mishahara hiyo, pia kuna basi la kisasa limeagizwa kwa ajili ya timu hiyo,” alisema.

Mtoa habari huyo alisema hatua ya MO kuichukua Simba kama mdhamini inakuja baada ya timu hiyo kucheza Ligi hiyo bila kuwa na mdhamini, kufuatia kumalizika kwa mkataba uliokuwepo kati ya timu hiyo na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -