Wednesday, January 20, 2021

MO DEWJI APAGAWA NA SIMBA

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA EZEKIEL TENDWA

WAKATI mashabiki wa Simba wakipata burudani ya kutosha kutokana na kandanda safi iliyoonyeshwa na wachezaji wao kwenye Tamasha la ‘Simba Day’, furaha ilikuwa mara dufu kwa mlezi wao, Bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’.

Katika tamasha hilo ambalo lilifanyika juzi Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya mashabiki wa Simba, kikosi chao kilicheza na Rayon Sport ya Rwanda na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mohamed Ibrahim ‘Mo’.

Mashabiki waliohudhuria walionyesha nyuso za kutojutia kutoa viingilio vyao, kutokana na kuridhishwa na uwezo wa wachezaji wao lakini kubwa ni kwa jinsi Mohamed Dewji ‘Mo’, alivyoonekana mwenye furaha kubwa.

Mo alianza kuonyesha furaha hata kabla ya siku yenyewe kufika, kwani kila mara alikuwa akiposti maneno ya kuhamasisha mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye ukurasa wake wa facebook.

Na hata siku ilipofika, mapema tu alianza kuposti picha zake akidai anajiandaa kwenda uwanjani na alipoingia kwenye uwanja alishangiliwa sana huku mwenyewe akionyesha furaha ya hali ya juu.

Muda wa ukaguzi wa timu aliambatana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba na muda mwingi alionekana akishangilia hata alipokwenda kuzindua Simba App, hali ilikuwa hivyohivyo.

Mo ambaye anataka kuweka hisa ya asilimia 51 (51%), amehusika kwa kiasi kikubwa kwenye usajili wa Simba wa msimu huu akimwaga fedha za kutosha zilizofanikisha kuwaleta akina Haruna Niyonzima, Emmanuel Okwi na wengine.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -