Friday, December 4, 2020

MO DEWJI: TUTAVUNJA REKODI ZOTE

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA WINFRIDA MTOI

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, amesema kuwa watarajia kuvunja rekodi zote katika kilele cha tamasha la klabu hiyo, maarufu Simba Day litakalofanyika kesho kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa na ule wa Uhuru, Dar es Salaam.

Kwa wiki yote hii, Wanasimba walikuwa wakifanya shughuli mbalimbali za kijamii kama sehemu ya shamrashamra zao tamasha lao hilo linalofanyika kila mwaka.

Hatimaye kesho ndio itakuwa kilele cha tamasha hilo na kwamba kunatarajiwa kuwa na matukio lukuki ya kuvutia, ikiwamo burudani ya nguvu kutoka kwa wanamuziki nyota hapa nchini, wakiongozwa na Naseeb Abdul ‘Diamond’.

Sambamba na hayo, tukio hilo litahitimishwa na mchezo wa kirafiki baina ya kikosi cha Simba na Vital’O ya Burundi, huku wachezaji wote, wapya na wale wa zamani wakitarajiwa kutambulishwa kwa mashabiki.

Akizungumzia tamasha hilo wakati wa mahojiano maalum na kituo cha redio cha Wasafi, MO Dewji alisema moja ya hitoria itakayoandikwa kesho ni kujaza viwanja vyote viwili, yaani Uhuru na Benjamini Mkapa.

“Katika kilele cha Simba Day, mwaka huu tutavunja rekodi zote za kujaza viwanja viwili, tumepata heshima kubwa ya kuwa na shabiki wetu Diamond Platinum ambaye ni msanii mkubwa anayejulikana duniani na Afrika nzima ambaye ametupa heshima ya kuja katika shughuli yetu,” alisema Mo.

Mo amewataka Wanasimba kujitokeza kwa wingi siku hiyo bila kuhofia sehemu ya kukaa kwa sababu watakuwa wanamiliki viwanja viwili na popote pale burudani itawafikia.

Kuhusu usajili, alisema wamefanya kwa kuzingatia michuano wanayoshiriki, ikiwamo Ligi ya Mabingwa Afrika, lengo lao kubwa likiwa ni kuingia hatua ya makundi na kusaka nafasi ya kutwaa taji hilo.

“Nakumbuka zile goli tano tano tulizofungwa katika Ligi ya Mabingwa, ndio sababu ya kuamua kuleta chuma cha ulinzi ambaye ni  Onyango (Joash), huyu ametangazwa beki bora kule kwao Kenya na mchezaji bora wa Ligi Kuu,” alisema.

Alieleza kuwa hata Larry Bwalya ni mchezaji ambaye hawakufanya makosa kumsajili kwa sababu hata kocha wa timu ya Taifa ya Zambia, Milutin Sredojević ‘Micho’, amemwagia sifa kwamba ni moja ya wachezaji bora.

Pia, alimsifia mshambuliaji wao mpya, Chriss Mugalu pamoja na wachezaji wao wengine, akiwamo Bernard Morrison, Luis Miquissone na wengineo.

Alifafanua kuwa klabu ya Simba imefikia hatua kubwa kwa sasa kwa sababu imeweza kusajili mchezaji ghari wa milioni 500, hivyo miaka inavyokwenda, watafikia malengo yao ya kiushindani Afrika.

“Hatujafanikiwa kutwaa ubingwa wa Afrika kwa miaka mitatu, lakini ndoto ziko pale pale kwa sababu kuna baadhi ya changamoto zinazuia ila tumefikia pazuri hadi kufikia kusajili mchezaji wa milioni 500 si padogo,” alisema.

Alisema mipango yao inalenga hadi timu ya wanawake, Simba Queens, wanaiandaa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake, hivyo nako watafanya usajili mzuri.

Kwa upande wake, Diamond alisema kuwa ana usongo wa kutumbuiza kwani hajafanya hivyo muda mrefu, akiahidi kutoa burudani ya nguvu kwa wapenzi wa Simba watakaofika uwanjani kesho.

“Sitatumbuiza muda mrefu, nina usongo sana, siku hiyo itakuwa balaa, kwanza naipenda timu, pili ninaithamini, kwanza ninavyoijua timu yetu, ikifika saa nne asubuhi, uwanja umejaa. Dunia nzima itakuwa ikitazama, itakuwa ni balaa,” alisema.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -