Wednesday, October 21, 2020

MO KUICHUKUA SIMBA KWA STAILI HII

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA ZAITUNI KIBWANA

HAKUNA namna, Bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’, lazima apewe Simba na tayari staili itakayotumika kufanikisha zoezi hilo la mabadiliko ya kiuendeshaji katika klabu hiyo ya Msimbazi imewekwa hadharani.

Akizungumza na BINGWA jana, Mjumbe wa Kamati ya Mabadiliko ya klabu hiyo, Mlamu Ng’ambi, alisema kuwa katika mkutano mkuu wa dharura utakaofanyika katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dar es Salaam Desemba 11, mwaka huu wanachama watapiga kura ya mabadiliko ya katiba ambayo yatatoa nafasi ya kupiga hatua kuelekea kwenye mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji.

Mlamu alisema katika mkutano huo, wanachama wanatarajiwa kupitisha uamuzi wa kubadilisha Ibara 49 (i-ii) ya katiba ya Simba na kuifanya ibara hiyo ya 49 kuwa na vipengele i-iii huku kipengele cha iv kikiwa na vipengele vingine a, b, c na d.

Sasa kipengele hicho cha 49 kinasomeka ‘Kuvunja au kufutwa kwa Simba’, uamuzi wowote wa kuvunja au kufutwa kwa Simba unahitaji theluthi mbili (2/3) ya kura za wanachama wote wa Simba watakaohudhuria mkutano mkuu ulioitishwa kwa dhumuni hilo.

Lakini, baada ya kuboreshwa ibara hiyo itasomeka uamuzi wowote wa kubadilisha mfumo, kuvunja au kufutwa kwa Simba unahitaji theluthi mbili (2/3) za wanachama wote wa Simba waliopatikana katika mkutano mkuu ulioitishwa maalumu kwa madhumuni hayo.

Hii inamaanisha kuwa neno kubadilisha mfumo litakuwa limeongezwa kwenye ibara hiyo na iwapo kipengele hicho kitapita kitakuwa kinatoa nafasi kwa klabu kuanza mchakato wa mabadiliko ya kiuendeshaji kama ilivyoainishwa na ibara hiyo kipengele cha iii ambacho kitakuwa na vipengele vidogo a, b, c na d.

Ni katika vipengele hivyo vidogo vilivyopo chini ya kipengele cha iii cha ibara mpya ya 19 ndipo mchanganuo wa namna klabu itaweza kubadilisha mfumo wake wa uendeshaji utakuwepo, vipengele hivyo vitasomeka hivi:-

(a) Mkutano mkuu wa wanachama unaweza kuitishwa kwa mujibu wa Ibara ya 22 na kufanya mabadiliko ya mfumo wa umiliki au uendeshaji wa Simba.

(b) Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji au umiliki wa Simba hayataathiri hadhi ya wanachama wote halali wa Simba isipokuwa hadhi hiyo itabadilika kuendana na mfumo stahiki wa mabadiliko yaliyofanyika. Uwiano wa thamani ya umiliki wa kila mwanachama katika mfumo mpya utajadiliwa na kamati ya utendaji kutokana na thamani ya klabu na uwekezaji.

(c) Mfumo mpya wa mabadiliko ya uendeshaji au umiliki wa Simba utarithi haki na mali zote pamoja na madeni na wajibu wowote uliokuwa chini ya Simba kabla ya mabadiliko.

(d) Mabadiliko ya umiliki au uendeshaji wa Simba yatamaanisha kuacha kutumika kwa katiba hii. Mkutano mkuu chini ya mfumo mpya utapitisha katiba mpya chini ya utaratibu wa haki ya kura za mfumo huo mpya.

Mlamu aliendelea kusema kuwa katika mkutano huo wa Desemba 11, utakuwa na ajenda zifuatazo; uhakiki wa wanachama waliohudhuria, kufungua mkutano, hotuba ya rais, kusoma na kujadili mapendekezo ya mabadiliko ya katiba, kupiga kura, majumuisho ya mapendekezo na kufunga kikao.

Mjumbe huyo aliongeza kusema kuwa wameandaa ripoti ya mabadiliko ya kurasa 54 ambayo watawasilisha kwa wanachama wakati wa mkutano huo ambao utatoa dira halisi ya mchakato wa mabadiliko ndani ya klabu ya Simba.

Katika hatua nyingine: Baraza la Wazee la Simba, limewahimiza wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mkutano huo utakaofanyika Jumapili hii jijini Dar es Salaam.

Katika taarifa ya Baraza hilo lililo chini ya Mzee Omari Mtika, limeweka wazi kuwa linaunga mkono mabadiliko ndani ya klabu hiyo kwa sababu wazee wanaamini ni muhimu kwa maendeleo ya timu yao.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -