Wednesday, September 30, 2020

MORRISON AMNG’OA KIGOGO YANGA

Must Read

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake ...

ZAINAB IDDY NA RAMADHANI HASSAN, DODOMA

KATIBU Mkuu wa Yanga, Dk. David Ruhango, amejiuzulu wadhifa wake huo alioushikilia tangu Novemba 11, mwaka jana, huku nyota wa timu hiyo anayewaweka roho juu Wanajangwani kwa sasa, Bernard Morrison, akitajwa kuchangia hilo.

Habari ambazo BINGWA imezinasa kutoka ndani ya Yanga, zinasema kuwa Dk. Rugango tayari ameshawasilisha barua ya uamuzi wake huo wa kujiuzulu jana kwa sekretarieti ya Wanajangwani hao.

Kati ya sababu ambazo BINGWA limetonywa kuchangia Ruhango kujiuzulu ni kile kilichodaiwa kutotimiza majukumu yake ipasavyo, hivyo kuwafanya baadhi ya wajumbe wa klabu hiyo kutokuwa na imani naye.

Imeelezwa kuwa wajumbe wengi wa Yanga walikuwa wakimshinikiza Ruhango kuachia ngazi, huku pia wakimtaka Mwenyekiti wa klabu hiyo, Dk. Mshindo Msolla, kutomng’ang’ania Katibu wao huyo.

“Tangu alipopewa majukumu ya Utendaji Mkuu, ameshindwa kuvaa viatu hivyo kwa sababu hakuna alichokifanya wala kusimamia kuhakikisha klabu inafanya kazi kwa umoja, lakini pia kuipa maendeleo,” alisema mtoa habari wetu wa ndani ya Yanga.

Habari za ndani zaidi, zinadai kuwa Dk. Ruhago amekuwa akikorofishana na baadhi ya wajumbe wa kamati za Yanga kutokana na kuchangia mgogoro uliotishia kuigawa klabu hiyo hivi karibuni.

Imedaiwa hata ule mgogoro uliotokana na picha zilizokuwa zikimwonyesha kigogo mmoja wa wadhamini wao, Kampuni ya GSM akiwa amepicha na wachezaji wapya wa Yanga, akiwamo Morrison, Ruhango alihusika.

Juu ya mgogoro huo, baadhi ya wajumbe wa kamati za usajili na ile ya mashindano, walikuwa wakipinga kitendo cha mwakilishi wa GSM kuonekana katika picha akiwa na wachezaji wao wapya baada ya kuwasainisha mikataba, jukumu walilotaka lifanywe na wao au viongozi wa Yanga

Kitendo hicho kiliifanya GSM kuandika barua ya kuachana na Yanga, hali iliyowavuruga Wanajangwani hao, wakifahamu kujitoa kwa wafadhili wao hao, waliowasajilia wakali kama Morrison na wengine, lingekuwa ni pigo kubwa kwao.

Baadaye pande hizo mbili zilikutana na kuweka mambo sawa na hivyo GSM kukubali kuendelea kuisapoti Yanga, tena safari hii wakiingia kwa kishindo, wakitangaza kumwaga mamilioni kukisuka upya kikosi cha timu hiyo.

“Hata lile suala la GSM kutaka kujiondoa ni Ruhago alihusika na wale wajumbe waliojiuzulu na wengine kuondolewa. Tulijua na yeye angejiweka pembeni, lakini alikataa ndipo baadhi ya wajumbe walipoamua kumshinikiza afanye hivyo,” alisema mtoa habari wetu huyo wa uhakika wa ndani ya Yanga.

“Kuna baadhi ya wajumbe walimweka kitimoto Msolla na kumtaka amvue madaraka (Ruhango) na wao wapo tayari kumlipa gharama za kuvunja mkataba wake ambao umesalia miezi minne tu kumalizika, lakini Mwenyekiti wao huyo aliomba wawe na subira ili mkataba wake utakapomalizika, asiongezwe tena,” alisema.

Mtoa habari huyo aliongeza: “Dk. Msolla aliwaambia wajumbe hao kuwa ataongea na Ruhago na kumshauri achukue uamuzi huo mwenyewe ili kuepuka fedheha ya kuondolewa, bila shaka ndicho kilichofanyika leo (jana).”

Gazeti hili lilimtafuta Ruhango jana ili kuzungumzia suala hilo la kujiuzulu kwake, lakini alikataa kusema lolote kwa madai hakuwa tayari kufanya hivyo.

Wakati huo huo, kikosi cha Yanga, kimetikisa Bungeni, jijini Dodoma jana, huku Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai, akimuulizia Morrison.

Timu hiyo ipo jijini hapa kucheza mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya JKT Tanzania kesho, ikiwa ni baada ya kuichapa Mwadui FC bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga Jumamosi ya wiki iliyopita.

Akiitambulisha timu hiyo, Spika Ndugai alitaka kufahamu alipo Morrison, akisema: “Ninao wageni kwenye gallery yangu (sehemu ya kukaa katika Bunge kwa wageni) na upande wangu wa kulia, na hawa sio wengine, ni viongozi wa Yanga. Naomba msimame viongozi wa Yanga (huku Wabunge wakishangilia).

“Gallery yangu ya kulia ni wachezaji wa Yanga na baadhi ya viongozi wa timu ya Yanga, karibuni sana hapa bungeni, tunafurahi sana kuwa nanyi, hili ni Bunge lenu, sasa mnaweza mkakaa.

“Waheshimiwa Wabunge wanauliza mchezaji mmoja tu, sijui Morrison, naomba asimame Morrison, yupo… yupo eeeeh, hayupo bwana, hayupo, hayupo. Naomba wale Waheshimiwa wa Simba wapeni makofi kidogo.”

Katika kunogesha utani wa jadi wa Simba na Yanga, Spika Ndugai alisema licha ya Wekundu wa Msimbazi kufungwa katika mchezo uliopita kwa bao 1-0, lakini watakapokutana tena, wanauhakika Wanamsimbazi wataibuka na ushindi.  

“Msisahau tu kwa Yanga ule mkuki mmoja, ule bado tunaukumbuka sana, tutakapokutana tena, mjiandae kisawasawa maana itarudi mikuki kadhaa,” alisema Spika huku Wabunge wakishangilia.

Previous articleYanga mzuka kama wote
Next articleMorrison amwaga mboga
- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

KISA KONA YA CARLINHOS… ...

NA ZAINAB IDDY BAO la Yanga lililofungwa na Lamine Moro juzi katika mchezo dhidi...

HUYU MUGALU ATAWALAZA WATU NA VIATU TU!

NA ONESMO KAPINGA HAKIKA sijapata utamu wa mshambuliaji mpya wa Simba, raia wa DR Congo, Chris Mugalu,kutokana na jinsi...

Wachezaji Gwambina wapewa muda

NA ZAINAB IDDY KOCHA wa timu wa  Gwambina, Fulgence Novatus, amesema amewapa muda wachezaji wake  ili aweze kutathimini kiwango cha...

Kisu amfunika vibaya Manula

NA ZAINAB IDDY KIPA  wa timu ya Azam, David Kisu, amemfunika Aishi Manula  wa Simba kutokana na kutoruhusu...

Zahera awapa Simba taji mapema

NA ZAINAB IDDY BAADA ya Gwambina kufungwa mabao 3-0 na Simba  katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -