Sunday, January 17, 2021

Morrison amwaga mboga

Must Read

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi...

NA ZAINAB IDDY

CHEZEA Yanga ya Dk. Mshindo Msola na GSM wewe! Hapana chezea kabisa kwani kwa mipango iliyowekwa na uongozi kwa kushirikiana na wafadhili wao hao, hakuna mchezaji ambaye atakubali kuwa nje ya kikosi hicho msimu ujao kama alivyobaini Bernard Morrison.

Baada ya sinema ya wiki kadhaa kuhusiana na majaliwa ya Morrison baada ya kumaliza mkataba wake na Yanga, hatimaye mchezaji huyo raia wa Ghana ameamua kumwaga mboga kwa kukata mzizi wa fitna kwa kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya ubongo wake.

Pamoja na Yanga kusisitiza kuwa Morrison alishasaini mkataba wa miaka miwili zaidi Machi mwaka huu baada ya ule wa miezi sita uliokuwa umalizike mwezi huu, bado wapenzi wa klabu hiyo walikuwa njiapanda, wakishindwa kuamini iwapo nyota huyo wataendelea kuwa naye msimu ujao au la.

Wasiwasi wao huo ulitokana na madai kuwa Simba walizungumza na mchezaji huyo na kumpa mkataba wa awali, wakisubiri amalize muda wake Yanga ndio wamalizane naye.

Na kati ya mambo ambayo yalikuwa yakiwaumiza vichwa watu wa Yanga kuhusiana na madai ya Morrison kwenda Simba, ni tambo za watani wao hao wa jadi ambao mara kadhaa walikuwa wasisitiza kuwa watawatoa machozi Wanajangwani hao.

Japo Wanamsimbazi hawakuwa wameweka wazi ni vipi watawatoa machozi watu wa Yanga, lakini kutokana na jeuri ya fedha ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’, Wanayanga walihisi huenda ni juu ya Morrison.

Mbaya zaidi, hivi karibuni Morrison amekuwa akiidengulia Yanga, ikiwamo kuwazimia viongozi na hata Kocha Mkuu wake simu, wakati wa maandalizi ya safari ya kwenda Shinyanga kuvaana na Mwadui ya huko.

Hatimaye Morrison ameamua kufunguka kila kitu kuhusiana na uvumi wa kutakiwa na Simba, ikiwa ni siku moja baada ya kudai kuna kiongozi wa Wekundu wa Msimbazi hao alimpa fedha kamna sehemu ya kumshawishi kutua katika kikosi chao.

Morrison alisema kuwa alipewa Dola 10,000 za Marekani ambazo alielezwa zimetoka kwa Rais wa Simba ambazo aligawana wakala aliyempelekea kwa kumpa Dola 5,000.

Na jana Mghana huyo aliendelea kupigilia msumari katika madai yake hayo, akifunguka kila kitu juu ya madai ya kushawishiwa na watu wa Simba ili atue Msimbazi mwishoni mwa msimu huu.

Maelezo yaliyotolewa na Morrison, yameufanya uongozi wa Yanga kuamua kupiga hodi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuishtaki Simba kutokana na madai hayo.

Yanga wameamua kufanya hivyo wakisimamia katika taratibu za kimkataba ambapo mchezaji anaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu yoyote pale tu anapokuwa amebakiza miezi sita katika mkataba na klabu yake, wakati nyota wao huyo akiwa ameshasaini kandarasi ya miaka miwili tangu Machi, kama wanavyodai viongozi wa Wanajangwani hao.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Wakili Simon Patrick, ndiye aliyeanika juu ya mpango wao huo wa kwenda TFF baada ya kuzungumza kwa kina na Morrison na kujiridhisha na maelezo yake, lakini pia kile alichodai ushahidi walionao.

Kupitia mtandao wa Yanga, Patrick, alisema kuwa hawawezi kulifumbia macho jambo ambalo mchezaji wao amelizungumza katika video iliyosambaa mitandaoni kuhusiana na kupewa fedha na mtu wa aliyedai ni Rais wa Simba.

“Morrison ameeleza kila kitu kilichojitokeza kati yake na watu aliowataja wanatoka timu nyingine, hivyo tumepeleka malalamiko yetu TFF rasmi na chombo husika bila shaka kitasikiliza kesi kutokana na ushahidi tulioupeleka.

“Ushahidi tuliopeleka umetoka kwa mchezaji mwenyewe baada ya kumuhoji na kutupa maelezo na vitu vingine alivyonavyo Morrison kuhusiana na jambo hili.

“Bila shaka, kama itathibitishwa juu ya madai

Yetu, hatua stahiki zitachukuliwa,” alisema Patrick.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Usiyoyajua sare ya Leicester, United

NI katika mechi ya Ligi Kuu ya England iliyomalizika kwa sare ya mabaon 2-2.-Man United wamemiliki mpira...

Eti Zidane anapangiwa kikosi!

IMEFICHUKA kuwa wachezaji waandamizi wa Real Madrid walikaa kikao na Zinedine Zidane kumwambia wachezaji anaopaswa kuwapanga na ndiyo maana timu hiyo imeshinda...

DIDA ASAINI IHEFU FC

Golikipa wa zamani wa Yanga na Simba, Deogratius Munishi ‘Dida’ amejiunga na Timu ya Ihefu inayoshiliki Ligi Kuu Tanzania Bara katika kipindi...

JDart Nation wapanga kutawala Africa

CHRISTOPHER MSEKENA MWANAMUZIKI na bosi wa JDart Nation, JDart, amesema miongoni mwa mipango yake kwa mwaka 2021 ni kuhakikisha...

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki za Ligi Kuu Tanzania Bara...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -