Wednesday, October 21, 2020

Mourinho acharukia benchi lake la ufundi

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

MANCHESTER, England

KWA kile kilichotokea juzi wakati Manchester United ikicheza na ‘vibonde’, Zorya Luhansk, ni wazi kocha Jose Mourinho ameanza kuonyesha makali yake pale Old Trafford.

Taarifa zilizoenea hivi sasa ni kwamba, mkufunzi huyo raia wa Ureno aligeuka mbogo hata kabla ya kuanza kwa mchezo huo baada ya kuona kikosi cha wapinzani wao kikiwa tofauti na kile alichopewa na benchi lake la ufundi.

Katika mtanange huo wa Ligi ya Europa uliochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, Man United walichomoza na ushindi mwembamba wa bao 1-0 licha ya kumiliki mpira kwa asilimia 70.

Wakati mchezo ukikaribia kuanza, Mourinho alimgeukia msaidizi wake, Giovanni Cerra na imeripotiwa kuwa wawili hao walipishana kauli.

Inadaiwa kuwa kocha huyo wa zamani wa Chelsea alimtupia lawama Cerra akidai kuwa ‘line-up’ aliyopewa na msaidizi wake huyo ilikuwa tofauti na kikosi cha Zorya Luhansk.

Katika kuonyesha hasira zake kwa kitendo hicho, Mourinho alitupa chini ‘laptop’ yake ambayo huitumia katika mbinu za kiufundi.

Baada ya mchezo huo Mourinho alisema: “Hata Paul Pogba alishtushwa na mabadiliko yaliyotokea na nataka wasaidizi wangu kuwa makini na taarifa zote.”

Mbali na hilo, Mourinho alimpongeza staa wake Wayne Rooney ambaye ndiye aliyetengeneza bao Man United lililopachikwa na straika Zlatan Ibrahimovic.

“Ni bonge la straika kuliko Juan Mata ambaye alicheza kama mshambuliaji wa pembeni,” alisema Mourinho.

Kwa upande wake, Ibrahimovic alidai kuwa kikosi chake hicho kinatakiwa kuamka baada ya kutotandaza soka la kuvutia katika mechi hiyo.

“Tulishinda na nafikiri tunaweza kufanya vizuri zaidi. Natarajia makubwa zaidi kutoka kwenye timu yetu hii,” alidai fowadi huyo wa zamani wa PSG.

Itakumbukwa kuwa Man United walianza vibaya mbio za kuwania ubingwa wa Ligi ya Europa wiki kadhaa zilizopita baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Feyenoord ya Uholanzi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -