Wednesday, October 28, 2020

MOURINHO AKIWAAMINI HAWA MBONA MAMBO POA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

LONDON, England

KWA sasa mambo yanaonekana kutokuwa shwari kwa kocha wa Mancheter United, Jose Mourinho, kutokana na mwenendo wa kusuasua ambao timu hiyo inauonesha katika michuano ya Ligi Kuu England.

Mpaka sasa Manchester United wapo nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi hiyo, wakiwa nyuma kwa pointi saba dhidi ya vinara wanaoongoza ligi hiyo,  Manchester City.

Hali hiyo ndiyo iliyosababisha kuwapo kwa tetesi zikidai kwamba Mreno huyo angefukuzwa mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini kitendo cha kuweza kutoka nyuma na kisha akaondoka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Newcastle pengine ndicho kilichoweza kunusuru kibarua chake.

Kutokana na hali hiyo, kunahitajika kufanyika mabadiliko ya haraka ili kuinusuru timu na kuna wachezaji nwatano ambao Mourinho wanaweza kufanya vizuri katika kikosi cha kwanza endapo ataamini.

Wafuatao ni wachezaji hao endapo Mourinho atawaamini wanaweza kumsaidia. 

  1. Marcus Rashford

Baada ya mechi dhidi ya  Newcastle, Mourinho alisikika tena akiwamwagia lawama mastraika wake na huku akifikia hatua ya kuhoji kama wana uwezo wa kuchezea klabu kubwa kama hiyo.

Hata hivyo, kiwango kilichooneshwa na Rashford wakati akiwa chini ya Kocha Louis van Gaal msimu wa 2015-2016 kinaonekana kupungua kutokana na jinsi Mourinho anavyoshindwa kuwatumia wachezaji chipukizi.

Jambo hili linadhihirika wazi kutokana na kwamba licha ya kufunga mabao mengi katika kipindi cha misimu miwili iliyopita, Rashford msimu huu amekuwa akinyimwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza, ambapo mpaka sasa ni mechi mbili alizoanza.

Rashford ni kipenzi cha mashabiki wa klabu hiyo ya  Old Trafford na mwenye uwezo wa kufika mbali, lakini Mourinho anaonekana kumfikiria kivingine.

Hata kiwango ambacho amekuwa akikionesha wakati anapotokea benchi ni cha hali ya juu kutokana na nguvu na uwezo wake wa kukimbia ambao umekuwa ukiwapa shida mabeki wa timu pinzani.

Licha ya mpinzani wake mkubwa katika kuwania namba, Alexis Sanchez, ambaye alisajiliwa kwa bei kubwa msimu uliopita, ameshindwa kuonesha aina ya kiwango alichokuwa nacho Arsenal na anaonekana kuwa ni hasara kwenye kikosi hicho cha  Mourinho.

Rashford ni aina wachezaji kama Kylian Mbappe na kama atapewa nafasi kulingana na umri alionao ili aweze kuonesha kipaji chake, anaweza kuibeba  Manchester United

  1. Paul Pogba

Licha ya kutowekwa wazi mvutano kati yake na Mourinho, lakini kuna kitu ambacho wengi watakuwa hawakifahamu.

Kwa sasa Mfaransa huyo anajichezea anavyojua yeye binafsi na si kwa lengo la kumsaidia kocha wala timu na ndiyo maana hadi sasa ameweza kufunga mabao mawili na kutoa pasi zilizosaidia kupatikana idadi kama hiyo.

Wawili hao wamekuwa katika mvutano na kocha huyo, tangu majira haya ya joto wakati zilipoanza kuwapo tetesi za kwamba Pogba anataka kuondoka na kwenda kujiunga na Barcelona.

Pogba alikuwa akicheza soka la hali ya juu chini ya Kocha Massimiliano Allegri, wakati akiwa  Juventus, ambapo alikuwa akiaminiwa zaidi na mkufunzi huyo na Mourinho atakapokuwa na mawasiliano mazuri na mchezaji wake huyo, badala ya kumlalamikia hadharani, hakuna wasiwasi kiwango chake kitarejea.

3 Eric Bailly

Msimu huu Chris Smalling na Victor Lindelof ndio wamekuwa wakiaminiwa katika safu ya ulinzi ya  Manchester United, lakini kiwango chao kimekuwa ni kibaya, wakati Bailly, ambaye anaonekana angeweza kufanya vizuri amepangwa mara tatu tu katika kikosi cha kwanza.

Tayari tetesi za kuhamia katika timu za Chelsea na  Arsenal zimeshaanza kwenye vyombo vya habari, lakini staa huyo bado ana muda wa kupata namba kwenye kikosi cha kwanza kwenye klabu hiyo ya  Old Trafford, naye pia endapo Mourinho atamuamini.

 4 Andreas Pereira

Baada ya kufanya vizuri katika michuano ya La Liga  akiwa na timu za Granada na Valencia kipindi cha misimu miwili, nyota huyo alihamia Old Trafford tayari akiwa na matumaini kuendelea na nafasi yake katika kikosi cha kwanza.

Hata hivyo, tofauti na matarajio yake, staa huyo amejikuta akichezeshwa kikosi cha kwanza mara mbili na huku akitokea benchi mara moja.

Mourinho amewahi kushusha viwango vya wachezaji akiwa na klabu mbalimbali kama vile  Mohamed Salah na Kevin de Bruyne, wakati wakiwa Chelsea na sasa hali hiyo inaonekana kumnyemelea Pereira.

Hii inatokana na kwamba baada ya kumsajili kwa gharama Fred kungeleta mabadiliko, lakini Mbrazil mwenzake huyo ameshindwa kulimudu soka la Uingereza na huku Mourinho akionekana kutomwamini kila mchezaji aliyepo benchi kama anaweza kufanya kitu tofauti.

5 Anthony Martial

Licha ya Martial kusemekana kuwa kati ya wachezaji bora Ulaya, lakini amekuwa hapangwi mara kwa mara.

Msimu wake wa kwanza katika michuano ya Ligi Kuu England aliweza kufunga mabao 11, lakini kwa sasa anaonekana kuvurugwa na Mourinho na mbinu zake za ufundishaji.

Mfaransa huyo kwa sasa ananyimwa nafasi kufuatia uwepo wa mastaa Alexis Sanchez, Fred, na Jesse Lingard, licha ya kuwa na kiwango kizuri.

Hapana shaka kwamba Martial anaweza kuongoza mashambulizi kuliko mastaa hao endapo atapewa nafasi.

Kutokana na kipaji chake, Martial ana uwezo wa kukimbia kukokota mpira, kitu ambacho kinatakiwa kwa Manchester United ili kuweza kupenya kwenye ngome ya wapinzani wao.

 

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -