Wednesday, October 28, 2020

MOURINHO AKUBALI KUMUUZA POGBA KWA PAUNI MIL 200/-

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

MANCHESTER, England


 

KLABU ya Manchester United na kocha wao, Jose Mourinho, hawataki kupepesa maneno. Kiufupi hawataki kupandwa na mtu yeyote kichwani hivi sasa.

Ripoti iliyotolewa na mtandao wa Daily Mirror ni kwamba, miamba hao wa soka England wameitaja thamani ya kiungo wao, Paul Pogba, kuwa ni pauni milioni 200.

Pogba anatarajiwa kutimka Old Trafford ifikapo Januari mwakani, huku uhusiano wake na kocha wa United, Jose Mourinho, ukizidi kufuka moshi wa hatari kufuatia uamuzi wa Mourinho kumpokonya Pogba majukumu ya unahodha msaidizi.

Uamuzi huo wa Mourinho ulifanyika baada ya Man United kulazimishwa sare ya bao 1-1 kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Wolves, wikiendi iliyopita.

Mara baada ya mchezo huo, mtandao wa The Sun ulieleza kwamba, Mourinho alimpa makavu Pogba katika chumba cha kubadili nguo, kutokana na kosa alilofanya uwanjani na kuwazawadia Wolves nafasi ya kusawazisha bao.

Hilo lilifuatiwa na lawama za Pogba kwa Mourinho, akiziponda aina ya mbinu za uchezaji zinazotumika na kocha wake huyo na sasa Mourinho anataka kumuuza kiungo huyo.

Mapema jana asubuhi, mtandao wa Sky Sports uliibuka na habari kubwa ya mtifuano kati ya Mourinho na Pogba, katika mazoezi ya timu hiyo, saa kadhaa baada ya United kung’olewa Carabao Cup na Derby County.

United ilifungwa kwa penalti 8-7 dhidi ya timu hiyo inayonolewa na Frank Lampard, mchezo ambao ulichezwa usiku wa kuamkia jana.

Taarifa hiyo iliambatana na video ambayo ilimwonesha Pogba akisalimiana na baadhi ya wakufunzi, lakini alipishana na Mourinho kama hamjui, kabla ya kusimama na ‘kumkata kijicho’ kocha wake huyo kwa kile kilichoonekana kuwa ni majibizano baina yao.

Ikumbukwe kuwa baada ya kumalizika kwa mechi dhidi ya Derby, Mourinho, alihojiwa na kukanusha uvumi wa kuwepo kwa bifu kati yake na Pogba.

Katika mchezo huo, Pogba hakucheza lakini alionekana akiwa jukwaani katika dimba la Old Trafford, lakini Mfaransa huyo aliamua kuondoka kabla ya kuanza kwa penalti.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -