Friday, October 30, 2020

MOURINHO AWEKA REKODI MBAYA KUPITA KIASI MAN UTD

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

 

LONDON, England


UNAWEZA kusema ni  majanga kutokana na matokeo mabaya mwanzoni mwa msimu kwa timu ya Manchester United kuyapata tangu msimu wa  1990-91, baada ya kuambulia sare ya  bao  1-1  dhidi ya  West Ham United.

Hali hiyo inatokana na kuwa klabu hiyo ya  Old Trafford  iliamua kumuajiri kocha wao, Jose Mourinho, msimu huu, baada ya miaka mitatu kukosa mafanikio ikiwa chini ya makocha  David Moyes na Louis van Gaal, lakini kocha huyo wa zamani wa  Chelsea ameshindwa kufanya kile kilichotarajiwa.

Hadi sasa Man United imeshakusanya pointi  20  kutoka katika mechi 13  ilizokwishacheza, idadi ambayo ni sawa na waliyoipata msimu wa  1990-91, wakati walipofikisha pointi  21 katika michezo kama hiyo 13, lakini idadi hiyo ikapungua baada ya kubanwa mbavu na  Arsenal.

Kutokana  na matokeo hayo ya mwishoni mwa wiki,  vijana hao wa Mourinho wapo nyuma kwa pointi 11 dhidi ya timu inayoongoza ligi hiyo, Chelsea na huku wakiwa nyuma kwa pointi nane dhidi ya timu inayoshika nafasi ya nne,  Arsenal  katika vita ya kuwania kushiriki kwenye michuano ya Ligi ya  Mabingwa.

Kiwango hicho kibovu cha Man United juzi kilimkasirisha Mourinho, ambapo Mreno huyo alijikuta akipelekwa jukwaani na mwamuzi, Jon Moss, baada ya kuonekana kuchanganyikiwa na uamuzi wa kupewa kadi ya njano nyota wake, Paul Pogba,  kwa kosa la kujiangusha ambapo kocha huyo alipiga teke chupa ya maji.

Hata hivyo, Mourinho ana matumaini kikosi chake kitazinduka na kuondokana na mwanzo mbaya wakati wiki ijayo kitakapofunga safari kwenda kuivaa  Everton.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -