Friday, December 4, 2020

MOUSA DEMBELE: MTOTO WA DEREVA ‘TAXI’ ANAYETAFUTWA NA FEDHA ZA MADRID, BAYERN

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

LONDON, England

MOUSSA Dembele si jina geni kwenye ulimwengu wa soka kwa sasa. Hata hivyo, kuna zaidi ya wachezaji wawili wanaotumia jina hilo barani Ulaya.

Ukiachana na wa Tottenham, ninayemzungumzia hapa ni yule anayekipiga katika klabu ya Celtic ya Ligi Kuu nchini Scotland.

Kwa sasa ni mmoja kati ya wachezaji wanaosakwa kwa fedha nyingi na klabu vigogo za barani Ulaya.

Real Madrid, Bayern Munich, Chelsea, Barcelona na Arsenal, ni miongoni mwa klabu tajiri zinazoshindana kuinasa huduma yake.

Hivi karibuni, Bayern ilitangaza kuwa iko tayari kutoa kitita cha pauni milioni 30 kumpeleka Bundesliga. Kiasi hicho cha fedha ni zaidi ya shilingi bilioni 81 za Tanzania.

Hata hivyo, kufikia mafanikio hayo haikuwa kazi nyepesi kwani Dembele ni miongoni mwa mastaa waliowahi kupitia maisha magumu.

Dembele aliwahi kuishi maisha ya kipato cha chini na kuna kipindi aliingia kwenye mizunguko ya watoto wa mtaani ‘machokoraa’.

Amewahi kukiri kuwa alijua angeweza kutoboa kimaisha hasa kutokana na uwezo mkubwa wa kucheza soka aliokuwa nao.

“Nafikiri ni zawadi kutoka kwa aliye juu (Mungu),” alisema nyota huyo.

“Kila nilipokuwa na nafasi, nilicheza soka mitaani na kaka zangu. Niligundua kabisa kuwa ningekuja kuwa mwanasoka. Niliongeza juhudi na kukaza zaidi kufika hapa nilipo. Nilipambana nilipokuwa nikicheza na kaka zangu na marafiki zao.

“Kuna kipindi nilicheza soka hadi usiku. Baba aliogopa nilipokuwa nikifanya hivyo. Tulicheza mpaka usiku, ni kwa sababu tulipenda soka.

Baba yake alikuwa na kibarua katika miradi ya ujenzi na kuna kipindi alikuwa dereva ‘taxi’.

“Nilitazama Ligi ya Mabingwa Ulaya sana. Mechi ninayoikumbuka ni ile fainali kati ya mwaka 2005 kati ya Liverpool na AC Milan.

“Ukiwa mtoto, halafu ukasikia wimbo wa Ligi ya Mabingwa kwenye televisheni, lazima utataka kuwa pale na kuwa sehemu ya wanaocheza. Hivi sasa ninaweza kufanya hivyo nikiwa na Celtic.”

Akiwa na umri wa miaka nane, Dembele alichukuliwa na ‘academy’ ya PSG na baadaye aliingia kwenye kikosi cha kwanza ambapo alishindwa kupata namba.

“Nilikuwa PSG tangu nikiwa na umri wa miaka nane. Nilipoanza nao, nilikuwa nafanya mazoezi mara mbili au tatu kwa wiki. Hiyo ilikwenda mpaka nilipofikisha umri wa miaka 12 au 13.

“Nilipofikisha umri wa miaka 13 nilianza kuishi kwenye academy. Pale ilikuwa ni mazoezi kila siku na kufikiria soka tu. Kwa hiyo, ilikuwa ni mchanganyiko wa soka nililocheza mtaani na lile la kitaalamu,” alisema Dembele.

Hata hivyo, Dembele alishindwa kubaki PSG kwa kile alichodai kuwa alikuwa na hamu ya kuingia uwanjani mara kwa mara si kuishia benchi.

Kitendo cha kukosa namba PSG kilimfanya kutimkia England ambako alijiunga na Fulham.

“Ulikuwa ni uamuzi mzuri kwangu. Niliiacha klabu ambayo niliichezea miaka nane. Ulikuwa ni uamuzi mzito. Lakini, ukiwa mchezaji unapaswa kuchukua uamuzi mgumu. Hata nilipohamia Fulham mamabo yalikwenda poa kabisa.

Dembele alitua Celtic siku chache baada ya kusherehekea ‘birthday’ yake ya kutimiza umri wa miaka 20 na aliyemsajili ni kocha wa sasa wa timu hiyo aliyewahi kuinoa Liverpool, Brendan Rodgers.

Nyota huyo aliwahi kukipiga Ligi Kuu England katika klabu ya Fulham.

Akizungumzia kitendo cha klabu vigogo barani Ulaya kuifukuzia saini ya mteja wake, wakala wa Dembele, Mamadi Fofana, alisema: “Moussa hana wasiwasi. Alisaini mkataba wa miaka minne hapa Celtic na kichwani kilichopo kwake ni kubaki Celtic kwa kipindi hicho.

“Kama atalazimika kuondoka itakuwa kwa wakati sahihi, lakini si kwa uamuzi wangu au wa Moussa,” alisema Fofana.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -