Friday, October 30, 2020

MPENZI ASIYETAKA UIGUSE SIMU YAKE NI JIPU HILO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

KARIBUNI ndugu wasomaji katika safu hii ya uhusiano wa kimapenzi ambayo huwa inawajia kila Jumanne na Jumamosi, ikitoa nafasi kwenu kufahamu na kuchangia mambo mbalimbali yahusianayo na mapenzi.

Awali ya yote, nitoe shukrani zangu za dhati kwa wote ambao walichangia mada ya wiki iliyopita iliyosomeka ‘Kuigusa simu ya mpenzi wako ni ulimbukeni?’

Ama kwa hakika, waliotoa maoni yao ni wengi mno kiasi cha kunipa faraja kuona Watanzania wanapenda kushirikishwa katika mambo kama haya.

Hiyo ndiyo imani yangu, naamini maoni ya wengi yanaweza kuwaelimisha zaidi wasomaji wangu.

 

Mmoja wa waliochangia mada hiyo, yupo mama mmoja ambaye hakupenda jina lake kuwekwa hadharani kutokana na nafasi yake ndani ya Serikali na jamii aliyenipigia simu na kuchangia kwa urefu sana akisema:

“Mimi ni mmoja wa waliojeruhiwa na simu, kwa sasa nimeshaachana na mume wangu kwani alikuwa analala nayo ubavuni, usiku kucha simu zinaingia na sms, siku moja nikaigusa nikakuta sms za mwanamke wake wa nje, kumbe mwezangu alikuwa na mwanamke mwingine ndio maana alikuwa hataki simu yake iguswe.

“Ukiona mwanamume anaidhibiti sana simu yake, ujue upo katika hatari kubwa, watu wasilichukulie hili kwa wepesi, kama unaweza kukaa kwenye nyumba ukafunga milango, madirisha kwa hofu ya kuibiwa fenicha na pesa, kwanini usililinde penzi lako ambalo ndilo linaloyalinda maisha yako hasa dhidi ya janga la Ukimwi?

“Kudhibiti penzi lako ni zaidi ya kuzilinda fedha kwenye mabenki au maduka. Lakini pia ukiona mtu anaifuatilia simu ya mpenzi wake, ujue kuna kitu amehisi, si bure na hapo lazima kutakuwa na kitu.”

Ukiachana na msomaji huyo aliyeonekana kuguswa mno na mada hii, wapo wengine walionitumia ujumbe mfupi wa maneno kama ifuatavyo:

“Kama una mpenzi wa aina hiyo anayepokea simu pembeni yako, asiyetaka ushike simu yake au anaizima pindi mnapokuwa wote, basi huyo si sahihi kwako katika suala la kimapenzi maana anaonyesha hana penzi la dhati kwako.” Amran wa Dar es Salaam.

“Ni kweli kwa upande mwingine ni ushamba, lakini kama kweli simu haina walakini, kwanini ukatae mpenzi wako aiguse? Kuchunguza simu ya mpenzi wako ni muhimu usije ikawa unaishi na muuaji, iweje apigiwe simu akapokelee nje, hafai kabisa.” Omari wa Kinyeto, Singida.

“Si ulimbukeni mpenzi wangu kuigusa simu yangu kwani nampa nafasi nzuri ya kuniamini na kama sitamruhusu kuigusa basi ndani ya simu yangu au ya mpenzi wangu kuna maasi nayaficha.” Samwel Daniel wa Mlandizi, Pwani.

“Kushika simu ya mpenzi wako si vizuri maana kila mmoja ana mambo yake, pia naweza sema ni vizuri kwasababu unaambiwa mtu chake.” Rehema Maganda ‘Mama Ashirazy’ wa Kimara Korogwe, Dar es Salaam.

“Kuchezea au kupokea simu ya mpenzi wako ambaye unatarajia kumuoa si ushamba ila kama mwenyewe hataki ufanye hivyo, hauna budi kuacha na kama anapenda haina shida.” Shafih Mkahekela wa Chawi, Mtwara Vijijini.

“Kukagua simu ya mpenzio ni ushamba, kumbuka unaweza kuikagua ukakuta sms ila haikuwa yake, mtu alikosea namba akawa ameituma kwa mpenzio, huoni utakuwa umemwacha umpendaye bila sababu? Pia kumbuka kukagua simu si sababu ya kumzuia mpenzio kuwa muhuni.” Gasper Missibo wa Mbezi kwa Yusuph, Dar es Salaam.

“Kiukweli mimi na mpenzi wangu tunaishi vizuri, suala la kugusa simu yake au yangu ni kawaida sana kwasababu kila mtu anamwamini mwenzake. Niwaombe walioolewa au kuoa wawape wanaume au wanawake wao uhuru wa kushika simu zao ili wawe na amani.” Daniel Magoma wa Musoma.

“Si ushamba wala ulimbukeni kugusa simu ya mpenzi wako, kwanza inaonyesha ni jinsi gani unampenda. Sisi wanaume ni wepesi sana kugusa simu za wenzetu, lakini yako ikiguswa tu unawaka, kwa hiyo basi tuaminiane.” Said Mapembe wa Mombo Sokoni, Korogwe.

“Kuwa mwili mmoja maana yake kuwa kitu kimoja kwa kila kitu, sasa kama kupokea simu anakimbilia nje, unadhani kuna uaminifu hapo? Wizi mtupu.” David Mlwale wa Makongo, Dar es Salaam.

“Penye mapenzi ya kweli lazima wivu uwe juu, hivyo si vibaya kuishika simu ya mpenzi wako na wala si ulimbukeni kama watu wanavyosema.” George Bundala wa ‘Rock City’ Mwanza.

“Kuchunguza simu ya mpenzi wako si ushamba ama wivu uliopitiliza, binafsi mpenzi wangu akiigusa simu yangu nafurahi kuona ni kiasi gani hataki kunipoteza.” Muyuga wa Musoma.

“Si ulimbukeni kugusa simu ya mpenzi wako kwasababu mpenzi wako ni mmiliki wa mawasiliano yako, ikijumuisha mawasiliano katika mambo yako ya furaha na huzuni, safari na marafiki zako. Ni haki yake kujua iwe ni kwa kuambiwa au kuchunguza mfumo mzima wa mwenzako.

Wanaokataa wapenzi wao kuguswa simu zao, roho zao zina rangi ya uovu, kwanini anakataa? Fikiria unauona mwili wako wote akiwa mtupu ila simu hataki, ukiona hivyo ujue hilo ni ‘jipu’.” Said Mwinyi wa Kunduchi Beach, Dar es Salaam.

“Kushika simu ya mpenzi wako si ushamba wala ulimbukeni, ni vizuri kwanza mkizoeshana hivyo hakuna mchepuko hapo, kila mtu atakuwa anamwogopa mwenzake, tena mimi ndio napenda na mchumba wangu ndio tabia yake na tunaenda sawa kuliko kila mtu simu yake iwe yake tu… hapo kamchepuko katatokea tu.” Moshy Yahaya.

Ndugu wasomaji, tukutane Jumamosi ambapo nitawaletea mada kali zaidi. Ahsanteni.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -