Monday, November 23, 2020

MPENZI WAKO ANAHITAJI UWE HIVI ILI AJIVUNIE ZAIDI KUWA NA WEWE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

TOKA tukiwa wadogo tumefunzwa kuishi maisha yasiyo na uhalisia. Ukiwa na hasira unakatazwa kuonesha hadharani hasira zako; wakubwa watakunasihi na kukwambia yaishe.

Ukiwa na chuki kwa mtu, rafiki ama wakubwa zako watasema si lazima chuki yako ionekane hadharani. Watakwambia si tabia njema kuonesha hasira zako dhidi ya wengine. Tumekuwa tukiishi katika maisha bandia kwa muda mrefu sana.

Hata baba ama mama akitaka kuongea na mtoto wake mdogo (mwenye umri wa kati miaka miwili ama mmoja) ataongea kwa kuigiza sauti ya kitoto. Huwezi kuona athari ya jambo hili kwa jicho la haraka. Ila ukweli hali hii inamjenga mtoto kuwa si mtu halisi. Anakuwa anaishi nje ya ukweli wake wa maisha. Anafanywa kuwa muoga na mtu asiye halisi sana.

Athari ya malezi haya imekuja mpaka katika maisha ya kimapenzi. Amini maneno haya, wapenzi wengi wana maneno na mambo mengi ya kufanya na wenzao ila wanaishia kujishauri wenyewe tu. Wanaogopa, akitaka kuzungumza anajikosoa, anawaza huenda akaonekana wa ajabu.

Wakati  mmoja akiwaza hivi, mwingine naye anawaza kama hivi; Kuwa na yeye kuna jambo anataka kufanyiwa, naye kuna jambo anataka kufanya ila anaogopa mwenzake atamuona wa ajabu.  Hii ni hatari inayoyakabili mahusiano mengi japo wengi wanaojiita wataalamu wa masuala ya mapenzi hawajawahi kuona hili.

Ijulikane binadamu kaumbiwa kuchoka na kukinahi. Katika suala la mapenzi, kitu kinachoweza kuwafanya wahusika wasichokane ni yale mambo mtu anayotamani kufanyiwa na mwenzake (fantansies). Hili ni suala linalokubalika kwa wataalamu wote wa masuala ya saikolojia ya mapenzi.

Inatajwa kuwa bila wapenzi kuwa huru kwa asilimia kubwa kwa wenzao, wahusika watakuwa wanaishi katika namna nusu ya ukweli wa hisia zao. Katika namna hii nusu, japo wanaweza kuonekana wakiwa na amani na furaha ila kiukweli amani na furaha yao haitokuwa timilifu. Ili kila mmoja aweze kufurahia mapenzi na mwenzake, ni jukumu la kila mmoja kuishi maisha yake kamili kwa mwenzake.

Mueleze mpenzi wako nini unapenda kutoka kwake. Mueleze nini unataka kufanyiwa. Kumuelezea huku sio tu inaleta furaha katika mazungumo yenu ila pia inatoa fursa kwenu ,kila mmoja kuwa huru na mwenzake.

Ni kufubaisha mahusiano yenu mkiwa mnaishi katika namna ya uoga. Eti mmoja anatamani kufanya hivi ama kufanyiwa vile ila anogopa kusema kwa kuhisia ataonekana wa ajabu.

Kwanza unatakiwa kujua, huna haja ya kuogopa kwa sbabau hata mwenzako naye ana jambo lake la kutaka kukwambia ila anasita kwa kudhani utamuona wa ajabu.

Kuwa huru, jiachie, mpenzi wako ndiye binadamu pekee anayetakiwa kujua ujanja na ujinga wako katika mapenzi. Hata kama utakaloongea litamshangaza ila ni vema akajua wewe ni wa namna gani na yeye atakwambi ni kwanini linamshangaza.

Kuishi kwa uoga, ama kwa kujidai una heshima mno kwa mpenzi wako hakutofanya lolote la maana zaidi ya kufubaisha hali ya mahusiano yenu.

Jiachie kwa mpenzi wako, huyo ndiye mwandani na mtu ambaye unapaswa kujiachia kwa kiwango cha juu zaidi. Kujiachia kwako kwake ndiko kutamfanya na yeye ajiachie kwako hali itakayowapelekea mfikie hatua muafaka ya kufurahia mapenzi yenu kiukamilifu na kuwaepusha kuchokana.

Wengi wanachokana katika mapenzi kwa sababu huishi kana kwamba wanapata maelekezo kutoka katika kitabu fulani cha kanuni. Maisha ya namna hii yanawafanya wahusika washindwe kuishi kutokana na msukumo wa hisia zao za kimapenzi na badala yake wanaishi kwa kuwaza kufanya mambo fulani wasionekane wa ajabu.

Mtaalamu mmoja wa saikolojia ya mapenzi aliwahi kusema kuwa; ili mapenzi ya wawili yazidi kuleta hamasa inabidi wakati mwingine wafanye vitendo ambavyo wakikaa na kufikiria wanabaki wanacheka na kusema sisi bwana.

Mahusiano ya wengi yanakosa hamasa na kufanya wahusika watoke nje ya mahusano yao, kwa sababu wanashindwa kuishi kiuhuru kihisia juu ya wenzao. Kila mmoja katika mahusiano ana jukumu la kumfanya mwenzake kuwa huru kusema, kutenda na kupendekeza lolote juu ya mwenzako. Hapo ndipo kila mmoja anaweza kuwa na hamu isiyoisha kwa mwenzake.

ramadhanimasenga@yahoo.com

 

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -