Friday, November 27, 2020

MPIRA MWEPESI ULAYA LAKINI MGUMU AFRIKA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA HONORIUS MPANGALA

SOKA ndio mchezo pendwa duniani kuliko michezo yote. Pamoja na kuwa na wapenzi wengi, soka limeweza kubadilika kwa kiasi kikubwa sana kwa kutazama nyakati zilizopita na leo hii.

Kwa miaka ya hivi karibuni soka la Ulaya limeonekana kubadilika usoni mwa watazamaji kulingana na aina ya mifumo inayotumika na timu na klabu mbalimbali Ulaya na maeneo Afrika, japo bado inaonekana kwa upande wa Afrika mabadiliko haya si makubwa sana kutokana na aina yetu ya mpira tunaoucheza kukingana na mzingira yetu.

Nataka kueleza kwanini soka linaonekana ni jepesi Ulaya na ni gumu kwetu Afrika, moja aina ya uendeshwaji wa timu au klabu Ulaya ni tofauti sana na ilivyo kwa uendeshwaji huo kwa timu na klabu barani Afrika.

Inawezekana tukasema miundombinu ya Kiafrika imekuwa changamoto lakini kuna mambo yanayohitaji uthubutu na roho ya kumjua Mungu katika kuendesha taasisi zinazohusu michezo au zile za umma.

Viongozi wa soka Ulaya weledi wao ni mkubwa sana kiasi kwamba wanakubali changamoto zinazoweza kuwakuta na hawajioni kama wao ndio wajuzi wa kila kitu, bali wanakubali kujifunza mambo ili kusaidia kusogeza maendeleo ya soka mbele, kwetu Afrika mara nyingi aliyeko madarakani kuendesha mpira basi atafanya kila njia ya kutaka tumwone bila yeye soka haliwezi kusogea lakini kumbe utendaji wa taasisi za umma zinazohusu jamii ya watu hauko hivyo.

Vitendo vya kutambua mahitaji ya msingi katika kulisukuma gurudumu la maendeleo ya soka na kutambua vipaumbele vya soka, ndivyo vinavyoweza kututofautisha kati yetu na wenzetu wa Ulaya na mwisho tunakuja kuona soka la Afrika ni gumu sana.

Kiuchezaji mpira hadi kufikia kumwona mchezaji anakupa huduma zilizo bora uwanjani, ujue kuna aina ya mtiririko wa matunzo mazuri yanayomgusa mchezaji moja kwa moja pamoja na benchi la ufundi, huku kukiwa na hali ya kuheshimu taaluma ya watu mnaowaamini mnawapa majukumu ya kuwavusha kutoka upande A kwenda upande B.

Aina ya uendeshwaji wa soka letu pamoja na aina yetu ya kufikisha maarifa kwa mchezaji ili akakupe kinachostahili ndani ya uwanja, nalo limekuwa jambo lenye mtihani mkubwa ambapo likikutana na mashabiki waliokunywa maji ya bendera ya klabu au timu husika, unakutana na maneno ya shombo dhidi ya mchezaji au benchi la ufundi.

Akili za mashabiki wa Kiafrika zinaenda mbali sana katika kulifuatilia soka la klabu zao ndani ya Afrika na timu za taifa kutokana na kulinganisha soka wanalolitazama Ulaya wakihitaji kuliona ktk klabu zao pendwa ndani ya Afrika, kitu ambacho kinaleta ugumu kutokana na miundombinu pamoja na aina ya malezi ya wachezaji wao yakiwa ya kuunga unga.

Wakati unataka kuiona Mbeya City ikipiga soka mujarabu kama inavyopiga Shakhtar Donetsk ya Ukraine, tujaribu kuangalia na miundombinu iliyoko huko tunakotaka kulazimisha tuone klabu zetu zitupe huduma kama ile tunayoifikiria.

Inawezekana ikawa ni ugonjwa wa Waafrika wa kugombea fito wakati wanajenga kibanda kimoja kama yale yaliyoko Zambia kati ya rais wa sasa wa FAZ na rais aliyetoka madarakani, wamekuwa na msuguano mkubwa sana ambao umetokana na uchaguzi uliopita.

Nani alifikiria kama rais aliyemaliza muda wake wa shirika la soka Ulaya, Michael Platin kwa alivyo mbobezi wa masuala ya soka kutokana na yeye kuwahi kuwa mchezaji, lakini watu walivyo waadilifu na wanavyojua kusoma nyakati pamoja na kukubali changamoto, wakitazama kila mmoja anaweza kuwafikisha wanakokusudia kulingana na mikakati yao.

Mtu kama Platin angekuwa yuko Afrika na akawa amepata nafasi ya kuongoza soka, sidhani kama angeweza kukubali kirahisi kuiacha nafasi ikaenda kwa mtu aliyekuwa nje ya duara la kiutawala kwa wakati huo.

Linaloshindikana Afrika wenzetu Ulaya wanaliweza na lile linaloshindikana Ulaya, linawezekana Afrika hii yote ni kutokana kuishi kwa kufuata misingi na taratibu za kiuendeshaji wa soka na wanaocheza.

Leo hii unaweza kuliona soka la Ulaya katika mifumo inayoeleweka lakini unaweza usione kwa soka la Afrika, kutokana na aina ya mapokeo ya wachezaji kwa sababu ya kuishi kwa mtindo wa mazoea unaotokana na wanaoendesha soka iwe klabu au timu za taifa, unapokutana na benchi la ufundi la Ulaya linakuwa lina watu wa kutosha tofauti na ilivyo kwa baadhi ya klabu za Afrika na ndio maana nafasi kama aliyokuwa nayo Hans van der Pluijm, ameweza kuiachia kutokana na kuona hakuna analolifanya na hi yote ni kutokana na miundombinu ya soka la Afrika hasa kwa klabu za Afrika Mashariki na Kati.

Nimalize na kuandika misingi bora ya uendeshwaji wa soka pamoja na hali ya kujitathmini kwa viongozi, ikiweza kuwaingia basi watakua wameweza kujibu akili za mashabiki wa Afrika kwa kutaka kuliona soka wanalolitazama Ulaya likaja Afrika kwa klabu zao pendwa na timu zao za taifa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -