Thursday, October 22, 2020

MRISHO NGASSA ATEMA CHECHE

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI


WINGA wa Yanga, Mrisho Ngassa, ameweka wazi kuwa hawana muda wa kusikiliza maneno ya watu zaidi ya kufanya kazi kuisaidia timu yao kupata matokeo mazuri katika mechi zinazowakabili za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yanga juzi ilifanikiwa kuanza vizuri ligi hiyo kwa kuifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA baada ya mchezo huo, Ngassa alisema maneno yapo siku zote na hayawezi kuathiri morali waliyoanza nayo kwenye ligi hiyo kwa wachezaji kujituma uwanjani.

Alisema kuwa, wameanza ligi hiyo wakifahamu watakutana na ushindani mkubwa kutokana na timu waliyocheza nayo kuwa na wachezaji wenye viwango, lakini malengo waliyoingia nayo yaliwasaidia.

“Maneno ya watu siku zote hayawezi kuharibu mipango tuliyojiwekea, waendelee kuongea, lakini sisi tunajua kazi yetu ipo uwanjani, tunataka kufanya vizuri msimu huu, tunashukuru kwa matokeo tuliyopata leo (juzi),” alisema Ngassa.

Akizungumzia siri ya ushindi wa kikosi chao, alisema ni mchezo wa kasi walioanza nao na kuwafanya wapinzani wao washindwe kuhimili kasi hiyo, licha ya kwamba hata Yanga kuna sehemu walizidiwa.

“Tumeona tulichokifanya leo (juzi) na Mwalimu alikuwepo, anajua wapi tulipokosea na atafanya marekebisho kabla ya mchezo wetu ujao, ninachowaomba mashabiki wa Yanga waendelee kutusapoti, tutapambana kwa uwezo wetu,” alisema Ngassa.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -