Wednesday, October 21, 2020

MSANII ALIYETELEKEZWA NA DIAMOND ANAVYOTAABIKA

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA JEREMIA ERNEST


 

MWAKA 2010 wimbo wa Nitarejea ulifunika na kutamba katika vituo mbalimbali vya redio na runinga nchini na nje ya mipaka ya Tanzania.

Wimbo huo uliimbwa na Nassibu Abdul ‘Daimond’ na kumshirikisha mwimbaji wa kike, Hawa Said Mayoko ‘Hawa Nitarejea’ na kuufanya utambe kwenye anga za Bongo Fleva.

Lakini Diamond ameendelea kufanya vizuri katika muziki huo, huku Hawa akiwa na hali mbaya kitandani.

Hawa ambaye ni mtoto wa tatu katika familia yake, ameshindwa kutoboa akidai ni baada ya Diamond kufanikiwa na kumtelekeza na kumsababishia msichana huyo msongo wa mawazo na kuingia kwenye dimbwi la unywaji pombe kupita kiasi.

Kutokana na kukosa kipato alijiingiza kwenye unywaji wa pombe za kienyeji mchanganyiko kama gongo, komoni na nyinginezo na kusababisha kuathirika kwa unywaji huo wa pombe wa kupindukia.

Unywaji huo wa pombe wa kupindukia ndio umemfanya awe taabani kitandani baada ya kupata ugonjwa wa ini na tumbo kujaa maji.

 

Maisha ya soba na ugonjwa

Baada ya kuathirika na unywaji huo wa pombe, mwaka jana alipoona maisha yake yanazidi kuwa magumu aliamua kwenda katika vyombo vya habari kujitangaza kuwa yeye ni mwathirika wa pombe.

Mkurugenzi wa Pili Missanah Foundation, Pili Misana, alijitolea kumchukua na kumlea akiwa mtoto pekee wa kike katika nyumba hiyo.

Baada ya muda hali yake ikaanza kuwa nzuri na kufanya kazi zake za muziki kidogo kama kutunga nyimbo na maandalizi ya kuingia studio, lakini ghafla mwanzoni mwa mwaka huu hali yake ilibadilika na kuanza kuwa mbaya tena.

Hawa alianza kupoteza hamu ya kula na tumbo lake kuanza kujaa gesi akaenda Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya kufanyiwa vipimo na kugundulika ini lake limekuwa kubwa na siku zilivyo zidi kwenda hali ilizidi kuwa mbaya na tumbo kujaa maji.

Alilazwa kwa muda wa mwezi mmoja akinyonywa maji na kwa mara ya kwanza alitolewa lita nne, ya pili lita tatu na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Kutokana na hali kuwa mbaya aliamua kurudi nyumbani kwao Buguruni Kisiwani huku tumbo likiendelea kujaa maji na waliporudi hospitali alitolewa lita nyingine nane za maji.

Daktari alimwambia ili apone inahitajika kuotesha ini ambapo utaalamu huo kwa sasa haujafika nchini, hivyo ataendelea kutolewa maji mpaka watakapoanza huduma hiyo.

Bingwa lilimtafuta mtaalamu wa afya, Obedi Kabinza, kufahamu sababu za ugonjwa huo na nini tiba yake.

Kabinza ni mkufunzi Chuo cha Sayansi ya Kinachohusiana na Afya (Decohas) kilichopo Dodoma, anasema sababu zinazosababisha ini kuwa kubwa zinaitwa (Hepatomegaly).

Sababu ya kwanza ni kuwa na uvimbe katika ini unaotokana na sehemu nyingine kuja kwenye ini ama maambukizi ya virusi viitwavyo Hepatitis A, B, C au E na hizo ni hatua za awali za uvimbe au hali ya ini kutofanya kazi vizuri kutokana na kuathirika (Cirrhosis).

Vitu vyingine vinavyoweza kusababisha ini kuwa kubwa ni matumizi ya pombe kwa muda mrefu, kutumia madawa bila ya mpangilio mfano kutumia dawa za maumivu mara kwa mara na moyo kushindwa kufanya kazi yake vizuri.

 

Tiba ya ugonjwa huo

Kabinza anasema tiba inategemea na ugonjwa ulionao, ila tiba kuu ni kuweka ini jingine ambalo utaalamu huo bado haujafika nchini labda Marekani, India na China.

Maombi yake kwa Watanzania

Kwa mtu yeyote anayeweza kumsaidia Hawa ili akapatiwe matibabu ya awali hapa nchini ama nje ya nchi anaweza kufika nyumbani kwao Buguruni Kisiwani karibu na ofisi za magari ya Taqwa.

Ama unaweza kuweka fedha kupita benki ya NMB 2031-0019560 pia unaweza kuwasiliana na mama yake kupiti simu ya mkononi 0712032705.

Mama wa msanii huyo, Ndagima Ramadhani, ameomba msaada kwa machozi kwa watu mbalimbali wanaoweza kumsaidia mwanawe akiwamo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli.

“Jamani naomba msaada wenu, naomba Rais Magufuli anisaidie ili mwanangu apate matibabu na hali yake irudi kama zamani,” anasema Ndagima.

 

Alipoanzia sanaa

Hawa alianza muziki akiwa mdogo alizaliwa mwaka 1990 katika Hospitali ya Isevya mkoani Tabora na kusoma Shule ya Msingi Ilala, Jiji la Dar es Salaam na kumaliza 2003 na hakuweza kuendelea na sekondari kwa sababu zilizo nje ya uwezo wake.

Kutokana na kupenda kuhudhuria katika bendi za muziki zilizokuwa zinafanya ‘show’ Ilala Ukumbi wa Vijana uliopo Amana, ambapo alikuwa akipata nafasi ya kupanda jukwaani na kuimba na kuonyesha uhodari.

Lakini siku zote Hawa alikuwa akipokea ushauri kutoka kwa rafiki zake kuwa aende akajiunge na Tanzania House of Talent (THT) na  mwaka 2005 alienda na kubahatika kupokelewa vizuri na Maunda Zoro pamoja na Mwasiti Almasi ambao ndio walimfanyia usaili.

“Nilipofika Mwasiti na wenzake walinifanyia usaili nikachaguliwa kujiunga nao, nikajaza fomu hapo ndipo safari yangu ya muziki ilipoanzia,” anasema Hawa.

Akiwa hapo alifanya kazi na wasanii watano ambao wote hawakuweza kutoka katika muziki na mwaka 2010 alikutana na Diamond Platinum na msanii huyo kuomba kumshirikisha kwenye wimbo huo wa Nitarejea na kumnadi kwenye soko la muziki.

Anasema baada ya wimbo huo kutamba katika anga ya muziki msanii huyo, Diamond hakuweza kumkumbuka tena kwa lolote ukizingatia hakuwahi kumkamilishia malipo ya kazi hiyo.

Mwaka 2012, Hawa alibahatika kuolewa na kupata mtoto mmoja wa kike aitwaye Luhaiya ambaye kwa sasa ana umri wa miaka sita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -