Saturday, November 28, 2020

MSIHOFU PESA IPO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HUSSEIN OMARI NA EZEKIEL TENDWA

KAMA ulidhani Yanga wapo vibaya kifedha utakuwa umekosea, kwani matajiri wa klabu hiyo wamewaondoa hofu mashabiki wao kwa kusema fedha zipo klabuni hapo.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya uongozi wa Yanga kutangaza kuachana na Mkurugenzi wa ufundi wa timu hiyo, Mholanzi Hans van der Pluijm na kueleza sababu kubwa ni kubana matumizi ya klabu hiyo.

Hali hiyo iliibua sintofahamu miongoni mwa mashabiki na wanachama wa klabu hiyo hasa kutokana na ukweli kwamba timu hiyo inakabiliwa na michuano ya kimataifa na pia kukabiliwa na ushindani mkubwa wa kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania.

Kutokana na sintofahamu hiyo, matajiri wa klabu hiyo wameibuka na kueleza wazi kwamba fedha zipo na mashabiki wasiwe na wasiwasi juu ya timu yao kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Zanaco ya Zambia utakaochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano wa Klabu ya Yanga, Paul Malume, ameliambia BINGWA si kwamba Yanga hawana fedha kama ambavyo imetafsiriwa na watu wengi kiasi cha kuzua taharuki kwa mashabiki wao.

“Mfuko wa Yanga uko vizuri, nawahakikishia hilo mashabiki, ndiyo maana sisi tunaendelea na mkakati wetu juu ya mikakati ya ushindi na kama kawaida wachezaji wetu wakishinda mifuko yao itatuna kwani fedha ipo,” alisema.

Malume alisema wachezaji wao wanatakiwa kuondoa shaka na kuendelea kujiandaa ili waweze kupata ushindi mkubwa utakaosaidia kusonga mbele kwenye michuano hiyo.

Alisema kama kuna watu wanadhani Yanga ipo taabani kifedha watakuwa hawajui lolote kwa kuwa klabu hiyo ni kubwa na ina matajiri wengi, ndiyo maana mpaka sasa hawajatetereka na wamepanga kuwafanyia makubwa wachezaji.

Malume ambaye yupo bega kwa bega na matajiri wa klabu hiyo kuhakikisha timu yao inapata ushindi mnono dhidi ya wageni wao, alisema wachezaji wao walitarajia kuingia kambini jana.

“Yanga ni timu kubwa ambayo ina watu wengi nyuma yake ndiyo maana unaona mpaka sasa hatujatetereka kwa chochote, tunapenda kuwapa taarifa mashabiki wetu kuwa tupo imara na leo (jana) timu inaingia kambini na itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa.

“Tunawaomba wachezaji wetu wasiwe na wasiwasi wowote, wao watulize akili na wafanye kweli dhidi ya Zanaco, wahakikishe wanashinda nyumbani na ugenini ili kuwatoa hao wapinzani wetu kwani mambo mazuri yanakuja,” alisema Malume.

Matajiri hao jana asubuhi walikuwa na kikao kizito na Kamati ya Utendaji ya timu hiyo kujadili mchezo huo wa keshokutwa pamoja na masuala mengine ya michuano ya ndani.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Seif Ahmed ‘Magari’, aliliambia BINGWA japokuwa hivi sasa hana wadhifa wowote katika klabu hiyo, lakini bado ataendelea kuwapa sapoti mabingwa hao.

“Naipenda Yanga japokuwa sina cheo chochote, lakini tupo pamoja na viongozi katika kupeana mawazo, ushauri na kila kitu,” alisema Magari.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Mkwasa kwa upande wake alisema watazitumia siku mbili zilizobaki za mwisho kuwajenga kisaikolojia wachezaji wa timu hiyo ambao wamekuwa wakisikia mambo mengi kupitia mitandao ya kijamii ambayo yamekuwa yakisambazwa na wapinzani wao.

“Wachezaji wamechoka, wamecheza mechi mfululizo mechi yetu na Zanaco ni muhimu, jopo la wataalamu wa saikolojia watakwenda kambini pale kuwaweka sawa kuelekea katika mchezo huo hasa kutokana na yale ambayo yamekuwa yakienezwa juu ya hali ya uchumi ya klabu,” alisema Mkwasa.

Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, amesema anaijua vizuri Zanaco ndani na nje, kwani licha ya kwamba ni mzaliwa wa Zambia, lakini pia amekuwa kocha wa Zesco United ya nchi hiyo.

Lwandamina alisema wanatarajia kupata upinzani mkali kutoka kwa wapinzani wao hao kwenye mchezo huo wa keshokutwa.

Zanaco wanatarajia kuwasili nchini leo wakiwa na kikosi kinachoundwa na Racha Kola, Mangani Banda, Toaster Nsabata, Ziyo Tembo, Peter Banda, George Chilufya, Fackson Kapumbu na Lee Ngoma.

Wengine ni Andrew Kwiliko, Taonga Bwembya, Saith Sakala, Charles Zulu, Ernest Mbewe, Richard Kasonde, Boyd Musonda, Augustine Mulenga, Aubrey Funga, Kwame Attram na Kennedy Musonda, tayari kwa mchezo huo.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -