Thursday, December 3, 2020

MSUVA: NGOMA, TAMBWE NI MUHIMU AISEE!

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA HUSSEIN OMAR

WINGA wa Yanga, Simon Msuva, amesema kukosekana kwa washambuliaji Amis Tambwe na Donald Ngoma katika kikosi chao kumesababisha kuondolewa mapema Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ngoma alishindwa kucheza mchezo wa marudiano uliochezwa juzi kwenye Uwanja wa Mashujaa, Lusaka na Tambwe alikosa mechi zote mbili dhidi ya Zanaco ya Zambia, kutokana na kuwa majeruhi, hivyo Wanajangwani hao kuaga kwenye michuano hiyo.

Zanaco imefanikiwa kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini, baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Yanga, katika mchezo wa kwanza uliochezwa Machi 11, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kabla ya juzi kutoka sare tasa.

Akizungumza na BINGWA jana, Msuva alisema Tambwe na Ngoma ni washambuliaji muhimu katika kikosi chao, kwani kukosekana kwao kimewafanya watolewe mapema Ligi ya Mabingwa.

Msuva alisema mechi kati yao na Zanaco ilimalizika nyumbani, baada ya kushindwa kupata ushindi mkubwa ambao ungewaweka katika mazingira bora ya kusonga mbele.

“Kila mchezaji ana umuhimu wake katika timu, tukubali au tukatae, tuna kikosi kipana, lakini hawa jamaa wawili ni muhimu sana kwetu,” alisema Msuva.

Alisema kutokana na matokeo hayo, hakuna sababu ya kuwalaumu makocha, ni mapema mno kufanya hivyo, kwani timu ilikuwa na majeruhi wengi.

Yanga ilifanikiwa kuingia mzunguko wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kuitoa Ngaya ya Comoro kwa jumla ya mabao 6-2.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -