Thursday, October 29, 2020

MSUVA: NIYONZIMA NI MPISHI WANGU

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA HUSSEIN OMAR

WINGA wa Yanga, Simon Msuva, amesema kiungo wa timu hiyo, Haruna Niyonzima, ndiye anayemwezesha kufunga mabao kutokana na pasi zake za mwisho.

Akizungumza na BINGWA jana, Msuva alisema uwezo wake uwanjani unachangiwa na Niyonzima kwani si mchoyo wa kumpa pasi.

Msuva alisema mabao yake mengi yanatokana na mchango mkubwa wa kiungo huyo, kwani amekuwa ni mpishi mzuri kwake kutokana na pasi za mwisho anazompa zinamwezesha kufunga.

“Naweza kusema Niyonzima ni moja kati ya viungo ambao wananiwezesha katika kunipa pasi za mwisho na kama utakuwa una kumbukumbu utaona mabao mengi ninayofunga napata pasi kutoka kwake,” alisema Msuva.

Msuva alisema ataendelea kufunga mabao kadiri atakavyoweza, licha ya kuzomewa mara kadhaa na mashabiki wa timu hiyo.

“Nitaendelea kushangilia kila nipofunga hata kama inatokea kuzomewa mimi sijali, nikiwafunga Simba au timu yoyote nitashangilia kwa kucheza kutokana napenda kufanya hivyo.”

Alisema amejipanga vizuri kuhakikisha anachukua tuzo ya ufungaji bora katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Msuva tayari amefunga mabao tisa sawa na Amissi Tambwe wa Yanga na Shiza Ramadhani ‘Kichuya’ wa Simba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -