Friday, December 4, 2020

MSUVA, NIYONZIMA WAITIKISA SONGEA

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

HUSSEIN OMAR NA EZEKIEL TENDWA


VIWANGO vilivyoonyeshwa na nyota wa Yanga, Haruna Niyonzima na Simon Msuva, vimeufanya Mji wa Songea, mkoani Ruvuma kutikisika baada ya mashabiki wa timu hiyo kuacha shughuli zao kwa muda kwenda kuwapokea vijana hao wa Jangwani.

Mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wameshawasili Ruvuma tayari kwa mchezo wao jioni ya leo dhidi ya Majimaji utakaochezwa kwenye Uwanja wa Majimaji.

Katika mchezo huo, Yanga watataka kupata matokeo mazuri ili kujitengenezea mazingira ya kuwatetemesha Simba waliopo kileleni mwa ligi hiyo.

Katika msimamo waligi hiyo, Yanga wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 40 kutokana na michezo yao 18, huku Simbawakitamba kileleni wakiwa na pointi 44.

Wachezaji ambao wanampa kiburi Kocha Mkuu wa Yanga, George Lwandamina, hasa katika safu ya ushambuliaji ni Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe na Simon Msuva ambao kila mmoja ana mabao tisa na kuwa kileleni kwenye orodha ya wafungaji mabao sawa na Shiza Kichuya wa Simba.

Ni kwa kufahamu mchango wa Msuva, Niyonzima pamoja na Tambwe katika kikosi chao, mashabiki wa Yanga wa Songea walionekana kuwatolea macho zaidi wakali hao na kutamani kupiga nao picha.

Akizungumza na BINGWA jana jioni, mmoja wa viongozi waliopo katika msafara wa timu hiyo, alisema: “Tumepokewa vizuri sana na mashabiki wetu wa huku ambapo wengi walionekana kuwababaikia Msuva, Niyonzima, Tambwe na hata Yondani (Kelvin) na wengineo.”

Kwa upande wake, Lwandamina alisema kila kitu kipo sawa na kwamba kumkosa Donald Ngoma na wenzake hakumuumizi kichwa kwani amewaandaa vizuri wachezaji waliopo.

“Ni kweli wapo wachezaji watatu ambao ni Ngoma (Donald), Zulu (Justin) na Chirwa (Obrey) ambao nitawakosa kutokana na majeraha, lakini hilo halitufanyi kuogopa na badala yake tunachohitaji ni kupambana kuondoka na pointi zote tatu,” alisema na kuongeza kuwa ameshangazwa na mapokezi waliyoyapata huko Songea.

Ngoma ambaye ni moja ya washambuliaji wa kutegemewa katika kikosi hicho, alikosa baadhi ya michezo ya michuano ya Kombe la Mapinduzi ukiwamo ule dhidi ya Simba walipolala kwa penalti 4-2.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -