Tuesday, October 27, 2020

MTAISOMA NAMBA

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINABU IDDY

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wamezidi kuchochea kasi yake katika mapambano ya kuwania  ubingwa wa msimu huu baada ya jana kuibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Stand United, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi, Sulemani Kinungani, kutoka Morogoro, mabao ya Yanga kwenye mchezo huo yalipachikwa wavuni na washambuliaji; Donald Ngoma, Simon Msuva, Obrey Chirwa na beki, Nadir  Haroub ‘Cannavaro’.

Yanga ilionekana dhahiri kupania kuvuna pointi tatu mwanzoni mwa mchezo huo, kwani dakika ya nne ilifanya shambulizi kwenye lango la Stand United lakini Cannavaro alishindwa kuunganisha wavuni pasi ya Msuva.

Baada ya hapo Yanga iliendelea kulisakama lango la Stand United, ambapo dakika ya nane, Msuva alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga lakini akapiga shuti dhaifu lililodakwa na kipa wa Stand United, Sebastian Stanley, huku dakika moja mbele, Chirwa akikosa bao baada ya shuti lake kupanguliwa na kipa wa Stand United.

Mashambulizi ya Yanga yalizaa matunda dakika ya 17 baada ya Ngoma kuifungia kwa kichwa bao la kuongoza akiunganisha krosi  ya Msuva.

Bao hilo ni kama liliiamsha Stand United ambayo dakika ya 23 ilifanya shambulizi ambalo hata hivyo halikuzaa matunda baada ya shuti la mshambuliaji wake, Abdul Aziz, kupaa juu ya lango la Yanga.

Dakika ya 26, Msuva aliiandikia bao la pili Yanga baada ya kupokea pasi ya  Ngoma na kuukwamisha mpira wavuni.

Dakika ya 32 kiungo wa Stand United, Selemani Kassim Selembe, alikuwa katika nafasi nzuri ya kuifungia bao timu hiyo lakini shuti lake lilidakwa na kipa wa Yanga, Deogratius Munishi.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika, Yanga ilikuwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku Yanga ikiingia kwa nguvu zaidi kutaka kujihakikishia pointi tatu muhimu kwa kupeleka mashambulizi kwenye lango la Stand United na kufanikiwa kuandika bao la tatu lililofungwa dakika ya 46 na Chirwa.

Dakika ya 49 kiungo wa Yanga, Justine Zullu, alikuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga baada ya kupokea pasi ya Ngoma, lakini shuti lake likapaa juu ya lango la Stand United.

Yanga iliendelea kutawala mchezo huo ambapo dakika ya 58 ilipata penalti baada ya Msuva kuchezewa rafu ndani ya eneo la hatari na Erick Mulilo.

Penalti hiyo ilipigwa na Msuva mwenyewe ambaye hata hivyo alikosa baada ya shuti lake kupaa juu ya lango la Stand United.

Yanga ilifanya mabadiliko dakika ya 60 ambapo kocha George Lwandamina, alimtoa beki Kelvin Yondani na nafasi yake kuchukuliwa na Vicent Andrew.

Pia kocha Lwandamina alifanya mabadiliko mengine dakika ya 65 ambapo alimtoa Ngoma baada ya kuumia na kushindwa kuendelea na mchezo na kumwingiza, Juma Mahadhi.

Mabadiliko hayo yaliiongezea nguvu Yanga na kufanikiwa kupata bao la nne dakika ya 68 kupitia kwa  Cannavaro aliyefunga kwa  kichwa baada ya kuunganisha kona iliyochongwa na  Juma Abdul.

Stand United nayo ilifanya mabadiliko dakika ya 75 ambapo alitoka kipa Sebastiane Stanley na kuingia Mohamed Makaka.

Dakika ya 78, Juma Abdul, alijaribu kupima uwezo wa kipa wa Stand, Makaka aliyeingia akitokea benchi lakini shuti lake lilionekana kuwa mboga baada ya kudakwa kilaini.

Yanga ingeweza kupata mabao zaidi kama washambuliaji wake wangekuwa makini ambapo dakika ya 79, Msuva aliwazidi kasi mabeki wa Stand United lakini krosi yake ilikosa macho baada ya mpira kutoka nje.

Stand United nayo haikuonekana kukata tamaa badala yake iliendelea kutafuta angalau bao la kufutia machozi kwani dakika ya 86, Frank Hamis, alipiga kiki kali iliyopanguliwa na kipa Dida.

Dakika ya 88, Msuva aliyepokea pasi ya Zullu nusura afunge bao lakini shuti lake liliishia mikononi mwa kipa wa Stand United.
Dakika ya 89, Vicent Andrew wa Yanga alionyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea rafu Jacob Massawe.

Hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika Yanga ilitoka kifua mbele kwa ushindi wa mabao 4-0.

YANGA: Deogratius Munishi 2. Juma Abdul 3. Haji Mwinyi 4.Nadir Haroub 5. Kelvin Yondani 6. Justin Zullu 7. Saimoni Msuva 8. Thabani Kamusoko 9. Donald Ngoma 10. Obrey Chirwa 11. Haruna Niyonzima/ Emanuel Martini (Dakika ya 58).

Stand United: Sebastian Stanley 2 . Erick Mulilo 3 . Adeyum Ahmed 4.Revocutus Richard 5.Jacob Massawe 6. Ibrahimu Job 7.Abull-Azizi Makame 8.Adama Salamba 9..Frank Khamis 10.Absalim Chidiebele / Amri Kiembe(Dakika ya 46) 11.Seleman Selembe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -