Wednesday, October 28, 2020

LWANDAMINA AANIKA MIFUMO YAKE HATARI

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

.Dozi za ‘wiki’ kurejea Jangwani

.Vigogo wakesha kuwatia ‘njaa’ Simba 


 

ZAITUNI KIBWANA NA HUSSEIN OMAR

UNAUFAHAMU mfumo unaozitesa timu nyingi duniani? Huo si mwingine, bali ni ule unaokwenda kwa jina la kitaalamu la Gegenpressing, yaani kukaba na kushambulia mwanzo mwisho.

Katika mfumo huo, mkiupora mpira kwa timu pinzani, mnahakikisha hawaupati na mkipoteza mnafanya kila linalowezekana kuunasa ndani ya muda mfupi.

Kwa wale ambao wamekuwa wakiiangalia Barcelona, mfumo huo wamekuwa wakiutumia zaidi kiasi kwamba hata timu pinzani inapokuwa na mpira, hujikuta katika wakati mgumu kuulinda kutokana na jinsi wachezaji wote wa wakali hao wa Catalan, wanavyohaha kuusaka.

Hata hivyo, mfumo huo huhitaji wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, pumzi, makini na wenye nidhamu ya hali ya juu ya mchezo.

Kwa hapa nchini, ni wachezaji wachache mno wenye uwezo wa kuhimili mfumo huo uliotamba duniani kwa takribani miaka mitano sasa, timu nyingine inayosifika kwa mfumo huo ikiwa ni Borussia Dortmund ambayo kama ilivyokuwa kwa Barca, ndio siri yao ya mafanikio kwenye michuano mbalimbali.

Lakini wakati wanasoka wa Tanzania wakionekana kukosa baadhi ya sifa za kumudu mfumo wa Gegenpressing, Kocha mpya wa Yanga aliyetangazwa mapema wiki hii, George Lwandamina, jana alizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya klabu hiyo na kuweka wazi kuutumia mfumo huo.

Iwapo wachezaji wa Yanga wataushika mfumo huo, ni wazi kuwa timu hiyo itakuwa ikigawa dozi za ‘wiki’ kama ilivyokuwa zamani, tena safari hii ikifanya hivyo hata dhidi ya timu kubwa.

Lwandamina alisema kuwa, anahitaji wachezaji wake kucheza soka la pasi za harakaharaka wanapokuwa na mpira wakati wanashambulia lango la timu pinzani, lakini pia kuwa wepesi wa kuusaka pale wanapoupoteza.

“Wachezaji wanatakiwa kujua wanaingia kwenye utamaduni mpya, hivyo naamini zaidi mfumo wa pasi za haraka haraka na kutoruhusu kushambuliwa kama ule mfumo wanaotumia Barcelona,” alisema.

Alisema kuwa licha ya mfumo huo, pia anapendelea mfumo wa kukaba na kushambulia pamoja (pressing game, counter pressing) ambao ameutaja kama chachu ya mafanikio yake alipokuwa na Zesco United ya Zambia aliyoifikisha nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu.

“Mfumo wa kukaba na kushambulia kwa kasi, ni chachu ya mafanikio kwa timu nyingi,” alisema.

Alisema kuwa ametua Yanga kupata changamoto mpya, kubadilisha ujuzi pamoja na kukipa maendeleo kikosi hicho kinachotarajiwa kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.

“Ni changamoto mpya kwangu, najua Yanga ni klabu kubwa, nitahakikisha ninatumia kila kinachowezekana kuhakikisha tunafanya vizuri, kuanzia kwenye ligi ya nyumbani hadi Ligi ya Mabingwa Afrika,” aliongeza.

Lwandamina, ambaye amechukua nafasi ya Mholanzi Hans van der Pluijm aliyebadilishiwa majukumu na kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, alisema kuwa lengo lake ni kuleta ujuzi mwingine ndani ya Yanga pamoja na kuipeleka Yanga kwenye hatua nyingine.

Akizungumzia suala la usajili, Lwandamina alisema: “Tayari Yanga ina wachezaji wake, hivyo sidhani kama hiki ni kipindi mwafaka kwa mabadiliko, nafikiri tutaendelea nao hawa hawa waliopo kwanza,” alisema.

Kwa upande wake, Plujim alisema hana mashaka na majukumu yake hayo mapya na kusisitiza: “Nitashirikiana vyema na Lwandamina pamoja na benchi zima la ufundi kuhakikisha tunatetea ubingwa wetu na kufika mbali kimataifa.”

Juu ya kambi, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga, alisema kikosi chao kitaanza mazoezi rasmi Jumatatu ya wiki inayoanza keshokuta kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili.

“Kuhusu kocha msaidizi, kwa sasa ataendelea kuwa Juma Mwambusi, Meneja Hafidh Saleh, huku kocha wa makipa akiwa ni Juma Pondamali na kama kutakuwa na mabadiliko, taarifa itatolewa,” alisema.

Lwandamina amekabidhiwa klabu ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikiwa na pointi mbili nyuma ya vinara, Simba, baada ya timu zote kushuka dimbani mara 15 katika mzunguko wa kwanza.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -