Monday, August 10, 2020

MTAKOMA Kazi imeanza, Hazard apandishwa mzuka Madrid

Must Read

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi...

MADRID, Hispania

TAA nyekundu imewashwa. Hatari inaweza kutokea muda wowote kuanzia sasa, baada ya kipa wa Real Madrid, Thibaut Courtois kuwapiga mkwara mzito wapinzani wao katika Ligi Kuu Hispania, La Liga, na Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Kipa huyo wa zamani wa Chelsea anaamini kikosi chao cha Real Madrid kitaanza kutamba kipindi hiki ambacho ligi mbalimbali zimerejea baada ya mapumziko ya kupambana na virusi vya corona.

Hata hivyo, Courtois amewaambia mashabiki wa Real Madrid kuwa staa wao mpya, Eden Hazard ndiyo atafanikisha kuiongoza timu hiyo kuelekea katika mafanikio hasa ya kushinda taji la La Liga.

Itakumbukwa Hazard hajaonyesha kiwango kizuri tangu alipojiunga na Real Madrid akitokea Chelsea kwa kitita cha pauni milioni 100.

Lakini Courtois anaamini huu ni wakati sahihi wa staa mwenzake wa timu ya Taifa ya Ubelgiji kuanza kuonyesha kiwango bora tangu alipoingia Santiago Bernabeu.

“Hazard yuko vizuri, si mchezaji ambaye anahitajika kuelezewa sana sababu ya kile alichokifanya England, lakini alikuwa na wakati mbaya mwanzoni mwa msimu hapa.

“Mambo anayofanya sasa kila mtu anashangaa, wote tunaamini atakuwa msaada mkubwa kuelekea kumaliza msimu huu wa La Liga ikiwezekana kushinda taji hilo.

“Kama akiendelea kuwa hivi, basi uhakika utakuwa mkubwa wa kushinda hata taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu huu au ujao, ni mchezaji wa daraja la juu ambaye anastahili kuvaa jezi ya Real Madrid,” alisema.

Hazard alilalamikiwa na mashabiki wa Real Madrid kwa kushindwa kufanya vizuri ndani ya kikosi hicho, katika kipindi cha miezi sita kabla ya ligi kusimama alicheza michezo miwili tu.

Real Madrid wamezidiwa pointi mbili na vinara Barcelona katika msimamo wa Ligi Kuu na wanatarajiwa kufungua pazia la La Liga kwa kucheza dhidi ya Eibar kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Hata hivyo, taarifa mbalimbali kutoka Hispania zinasema klabu hiyo yenye maskani yake katikati ya Jiji la Madrid itatumia kiwanja chao cha mazoezi cha Alfredo Di Stefano kucheza michezo iliyobaki ya Ligi Kuu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Klabu zamiminika kuomba kutumia U/Nelson Mandela

NA ASHA KIGUNDULA UONGOZI wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), umesema umeanza...

Kipa mpya Azam atamba kumsaulisha Abarola

NA ZAINAB IDDY KIPA mpya wa Azam, David Kissu, ameuahidi uongozi na mashabiki wa timu hiyo kuwa atajituma na...

Yanga: Hatuna mpango na wasugua benchi Msimbazi

NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Yanga, umesema hauna mpango wa kusajili wachezaji wanasugua benchi katika klabu ya Simba kwa...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...

TSHISHIMBI KUMFUATA MORRISON SIMBA

NA ZAINAB IDDY KIUNGO wa Yanga, raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi, anatarajiwa kumfuata winga wa kikosi hicho, Bernard...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -