Thursday, October 22, 2020

MTAMBO WA KUZALISHA VIPAJI KUTUA JANGWANI

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

HUSSEIN OMAR NA SALMA MPELI


JE, unajua ni jina gani limechomoza kufanya kazi na kocha mkuu mpya wa mabingwa watetezi Ligi Kuu Bara Yanga, George Lwandamina, akiwa msaidizi wake?

Ana sifa ya kutengeneza wachezaji mifano mizuri ikiwa ni Shiza Kichuya, Muzamiru Yassin na Mohammed Ibrahim ‘Mo’ wote ambao wanakipiga Simba.

Anayependekezwa kufanya kazi kwa karibu na Lwandamina ni Mecky Mexime, beki wa kulia ambaye pia ni nahodha wa zamani wa Mtibwa Sugar na timu ya Tanzania, Taifa Stars.

Mexime ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa Kagera Sugar, anatarajia kuchukua nafasi ya Juma Mwambusi aliyekuwa msaidizi wa Hans vander Pluijm.

Habari zilizopatikana jana ndani ya klabu hiyo, zilieleza kwamba Yanga wanatarajia kumwajiri Mexime ili aweze kusaidiana na Lwandamina kutokana na mafanikio ambayo kocha huyo mwenye umri mdogo Ligi Kuu Bara ameipata akizifundisha Mtibwa Sugar na Kagera Sugar.

Mtoa habari wetu alisema Mexime atajiunga na Lwandamina raia wa Zambia wakati wowote kuanzia sasa katika mazoezi ya timu hiyo yanayotarajiwa kuanza Jumatatu ya wiki ijayo.

“Mexime ana nafasi kubwa ya kuwa kocha msaidizi, hii inatokana na sifa alizonazo akiwa anaifundisha Mtibwa Sugar na sasa Kagera Sugar,” kilisema chanzo chetu.

Alipotafutwa na BINGWA, Mexime hakutaka kukanusha wala kukubali taarifa hizo, isipokuwa alisisitiza ni mapema mno kulizungumzia suala hilo kwa sababu yeye bado ni mwajiriwa wa Kagera Sugar.

“Sina cha kusema kuhusu taarifa hizo ukizingatia bado nina mkataba na Kagera Sugar, ila kama zipo (taarifa hizo) zitajulikana tu, hii dunia haina siri, tusubiri,” alisema Mexime.

Aidha, BINGWA lilimtafuta moja ya wachezaji wa Kagera Sugar kutaka kujua kama wamepewa taarifa zozote za kocha kuondoka kutokana na likizo zao kukatishwa ghafla.

Mchezaji huyo ambaye jina tunalihifadhi, alisema tangu warudi kwenye kambi yao Jumanne, wapo pamoja na kocha wao kwenye mazoezi na hajaonyesha dalili yoyote ya kuondoka.

“Hilo suala hata mimi nimelisikia tu watu wakizungumza, lakini kocha mwenyewe hajaweka wazi na tulikuwa naye kwenye mazoezi tangu juzi na leo (jana) asubuhi, wala hajaonyesha dalili ya kutuaga kama anaondoka,” alisema mchezaji huyo.

Katika hatua nyingine, Nahodha wa zamani wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, huenda akalamba shavu la kuwa meneja wa timu hiyo akichukua mikoba ya Hafidh Saleh ambaye atapewa cheo cha uratibu wa timu.

Nsajigwa aliliambia BINGWA kuwa hafahamu lolote kuhusu mpango huo, lakini kama lipo anashukuru kuona kuwa bado mchango wake unahitajika ndani ya Yanga.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -