Friday, September 25, 2020

Mtengenezee mwenzako pepo ili akikusaliti ajitie mwenyewe motoni

Must Read

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi...

NATAKA kuzungumzia usaliti. Hili ni suala la kipekee na  nyeti.  Umewahi kusalitiwa? Usaliti unauma sana. Usaliti unasononesha sana. 

Usaliti unavunja sana moyo. Mtu akisalitiwa anajiona mjinga, hana hadhi na mwenye mapungufu mengi. Baadhi huamua hufikia kufanya maamuzi magumu.

 Kuna mtu baada ya kusalitiwa alidhuru watoto aliozaa na mwanaume wake. Mwingine baada ya kusalitiwa alimmwagia mwanaume husika maji ya mto. 

Wote hawa walifanya matendo ya kijinga na ya kikatili sana. IIa unajua usaliti wewe? Uchungu wa mtu aliyesalitiwa huamsha hisia za hasira na ghadhabu.

Bila kupata msaada wa haraka mtu huyu anaweza kushangaza dunia kwa mamuzi ambayo anaweza kuchukua. Kama hujawahi kusalitiwa na mtu umpendaye kwa dhati, Sali sana, kuwa sana makini ili hilo suala lisitokee.

 Ila kuna watu wa aina mbili wanaosalitiwa. Wapo wanaosalitiwa kwa sababu watu walio nao wameendekeza tu tamaa. 

Na wapo wanaosalitiwa kwa sababu mazingira ya kusalitiwa wameyaandaa wenyewe. Jiulize, mtindo wako wa maisha haumfanyi mwenzako aone ana sababu ya kukusaliti. 

We mwaname kila siku unasema umechoka, humjali mumeo wala humuheshimu. Katika mazingira hayo akikusaliti utasema nini?

Mwanaume wako anahitaji faraja na raha kutoka kwako. Ila wewe unaendekeza marafiki na shughuli za kila siku. Mwenzako muda wa kutaka kukaa na wewe na kufurahia mapenzi yenu, wewe unafunga safari ya kwenda kwa kina Aneth.

 Akikusaliti utasema wanaume wabaya? Ili ujivue lawama katika usaliti wa mwenzako hakikisha unafanya yote unayotakiwa kufanya. 

Hakikisha unakuwa mstaarabu, mpole, chanzo chake cha furaha, raha na burudani katika maisha yake. Jiulize, unafanya hayo kwa uhakika na inavyotakiwa?

 Unakuta mwanaume hamjli sana mke wake. Yeye anadhani cha thamani cha kumpa mkewe ni fedha ya matumizi, pesa ya saloon na nguo tu? 

Hajali raha zake, hajali shida zake wala hajali huzuni yake. Katika namna hii, mwanamke huyu akidhani Joseph anaweza kumpa raha sana kuliko wewe Jackson unadhani kosa ni la nani?

Usaliti ni mbaya sana. Ila kabla hujamtukana msaliti hakikisha wewe sio chanzo cha usaliti huo. Jiulize kwa makini unatimiza majukumu yako kwa mwenzako kiuhakika?

Kila unachotakiwa kukifanya vizuri unakifanya?  Mpeni yanahitaji muongozo. Usiache mapenzi yaende yenyewe kama gari bovu. 

Ili mwenzako aione thamani yako inabidi uioneshe kwake. Ili mapenzi yasababishe raha na faraja baina yenu inabidi uwe chanzo cha hiyo raha na faraja. Unayafanya haya?

 Mapenzi ni sanaa. Na hakuna sanaa yoyote duniani ikosayo ufundi. Wewe ni fundi katika sanaa ya mapenzi kwa mwenzako?

 Ili kumuweka mbali na usaliti mwenzio, acha kumtafutia walinzi. Acha kuchunga sana simu yake, acha kumbana sana hata akakosa amani. Fanya hivi.

Mpe anachotakiwa kupata. Mpe raha ambayo hajawahi kuipata. Suuza roho yake itoke kutu na mateso ya maisha. Baada ya hapo, angalia kama ana uwezo wa kufanya kinyume na makubaliano yenu.

Asilimia kubwa ya wanaume wana amini wanawake ndiyo chanzo cha usaliti huku wakisahau jnsi wanavyosababisha usaliti huo.

 Unakuta mwanaume anajiona yuko bize na kazi na marafiki. Yeye  ni mtu wa kujali zaidi kuridhika kwake kuliko anavyojali ridhiko la mwenzake. 

Katika hali hii hudhani kama unachochea utoaji wa mbegu ya usaliti kwa mwenzako? Kila bindamu anapenda raha, amani na starehe. 

Kama ni wewe tu ndiye unadhani unastahili raha na amani, jua ipo siku utalia.  Ili mahusiano yalete thamani kwa kila mmoja, inabidi wahusika wajibidiishe kuwa wabunifu katika kukatana kiu zao.

Ifahamike hakuna mgomvi anayeanza ugomvi bila kuwa na hasira. Jiulize, unafanya nini ili usiwe chanzo cha kuamsha hisia za usaliti kwa mwenzako?

Wanaume wengi wanasalitiwa kwa sababu ya kuendekeza dharau katika mahusiano yao. Unakuta mtu hana hata muda wa kukaa na mpenzi wake na kufurahi, mtu hataki hata kutoka ‘outing’ na mpenzi wake ila anatoka na rafiki zake. 

Unadhani mke wako hataki kutoka ‘outing’ na wewe? Unadhani mkeo anajisikije akiona unatoka ‘outing’ na rafiki zako huku yeye umemuacha ndani kakaa tu?

 Yale uliyokuwa unayafanya katika uchumba wenu hutakiwi kuyaacha baada ya kuingia katika ndoa. Tambua, ule msisimko uliokuwa unatokea wakati mko katika hatua za mwanzo za uchumba wenu ulitokana na matendo yako juu ya mwenzako. Sasa kwanini unayaacha?

Mwenzako akiona unaacha kumthamini sasa wakati ulikuwa ukimthamini zamani atajua umepata mwingimne wa kumpa yale matendo yako mtamu. Akiwa katika fikra hizi unadhani kitu gani kitafuatia?

 Mwanamke acha kuchochea hisia za usaliti kwa mwenzako kwa kuwa mbunifu na makini na mpenzi wako. Acha kuishi kimazoea. Mapenzi ni sanaa. Na sanaa haikamiliki bila kuwa na ubunifu. U mbunifu wa kutosha ili uboreshe mahusiano yako?

Unaweza kupunguza na hatimaye kuzuia kabisa mwenzako asikusaliti ikiwa utayatekeleza majukumu yako kwa mwenzako ipasavyo. Jaribu kuwa mchoyo wa matendo ya hovyo kwa mwenzako kisha kuwa mtoaji wa matendo ya thamani na maana kwa mwenzako. fanya hivyo kwa ukuaji wa mapenzi yako. fanya hivyo kwa thamani ya mapenzi yako. fanya hivyo kwa heshima na hadhi ya mapenzi yako.

Instagram: g.masenga

 Mwandishi wa makala haya ni mtaalamu mbobezi wa masuala ya ushauri wa uhusiano, maisha na utulivu wa hisia ( Psychoanalyst)

   HYPERLINK “mailto:ramadhanimasenga@yahoo.com” ramadhanimasenga@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Azam FC yakiri Mbeya City kiboko

NA WINFRIDA MTOI LICHA ya kuchukua alama tatu kwa Mbeya City, uongozi wa Azam...

Niyonzima ala kiapo mechi za ugenini

NA ZAINAB IDDY NAHODHA msaidizi wa Yanga, Haruna Niyonzima, amesema kuwa mipango ya timu yao ni kuwa na mwendelezo...

Yanga achana nao

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga umekuja na mkakati maalum wa kuhakikisha wanakusanya pointi tatu kila mchezo, wakianzia mechi...

CHAMA GUMZO KILA KONA

NA WINFRIDA MTOI KIWANGO kilichoonyeshwa na kiungo wa Simba, Clatous Chama katika mchezo wa juzi wa Ligi Kuu Tanzania...

United ‘kimeo’ yamtoa povu Evra

MANCHESTER, EnglandBEKI wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra, amekerwa na namna mambo yanayoendelea katika klabu hiyo, hasa ishu za usajili.
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -