Sunday, October 25, 2020

MTIBWA KUANZA KUPUNGUZA DENI WIKI HII

Must Read

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian...

NA SALMA MPELI


UONGOZI wa Mtibwa Sugar, kupitia Mkurugenzi wake Mkuu, Jamal Bayser, unatarajiwa kuanza kulipa deni lao kwa timu ya Santos ya Afrika Kusini wiki hii.

Akizungumza na BINGWA jana, Bayser alisema wamekubaliana kulilipa deni hilo kwa awamu tatu tofauti na kulimaliza, kabla ya kuanza kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Mtibwa ilifungiwa kushiriki michuano hiyo baada ya kushindwa kukipeleka kikosi chao mwaka 2003 kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ni baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 kwenye mechi ya awali jijini Dar es Salaam.

“Tunatarajia wiki hii kuanza kulipa awamu ya kwanza ya deni letu, ili kulimaliza mapema kabla ya michuano ya Shirikisho haijaanza,” alisema Bayser.

Mtibwa wanatakiwa kulipa Dola 15,000, ambazo ni sawa na Sh milioni 34 za Kitanzania, kwa ajili ya fidia dhidi ya timu ya Santos.

Katika hatua nyingine, Bayser alisema kikosi cha Mtibwa kinatarajiwa kuondoka leo kwenda Mwanza kwa ajili ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba.

Mtibwa, ambao ni mabingwa wa kombe la Azam Sports Federation Cup (ASFC) na Simba ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu Bara, zinatarajiwa kushuka dimbani Jumamosi hii kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini humo, katika mchezo wa kuashiria kufunguliwa rasmi kwa pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, inayotarajiwa kuanza Agosti 22, mwaka huu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Fati aweka rekodi Barcelona

CATALUNYA, Hispania ANSU Fati ameweka rekodi ya mchezaji kinda wa kwanza kufunga mabao...

Lampard amshika mkono Silva

MANCHESTER, England KOCHA wa Chelsea, Frank Lampard, amesema atamtumia, Thiago Silva, katika mechi nyingi msimu huu licha ya kuwa na umri wa miaka...

Tuchel awatolea uvivu Mbappe, Neymar

PARIS, Ufaransa KOCHA wa PSG, Thomas Tuchel, amechukizwa na kiwango kibovu walichoonyesha mastaa wa timu hiyo, Kylian Mbappe na Neymar, kwenye mechi...

IBRA:Kifaa kipya Konde Gang aliyetembea kwa mguu kumwinda Harmonize

NA BRIGHITER MASAKI UKITAJA vijana wanaofanya vizuri katika mziki wa bongo fleva, huwezi kukosa kumtaja msanii chipukizi anayefahamika zaidi...

Jay-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas

-Z: Mama aliingilia bifu langu na Nas New York, Marekani HAKUNA shabiki wa Hip hop asiyelifahamu...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -