Friday, December 4, 2020

Mtibwa Sugar kuisimamisha Azam Uwanja wa Jamhuri?

Must Read

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

NA ASHA KIGUNDULA

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam wanatarajiwa kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo utakaochezwa leo kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro.

Kwa sasa Azam wanaongoza katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 21, baada ya kushinda michezo saba mfululizo tangu msimu huu, ulipoanza Septemba 7, mwaka huu.

Azam ambayo ipo chini ya kocha raia wa Hispania, Aristica Cioaba, wataingia uwanjani wakihitajia kuendeza ushindi katika mchezo wa leo ili waweze kubaki kileleni mwa ligi hiyo.

Katika mchezo huo, Cioaba anatarajiwa kuwatumia wachezaji mahiri akiwamo Mzimbabwe Prince Dube, anayeongoza kwa ufungaji wa mabao.

Kwa upande wa Mtibwa Sugar wataingia uwanjani wakiwa na malengo la kupata pointi tatu, baada ya kufanya vibaya baadhi ya michezo ya ligi hiyo.

Mtibwa Sugar ambayo kwa sasa ipo chini ya kocha msaidizi Vicent Banabas  baada ya Zuberi Katwila kuondoka na kwenda kujiunga na Ihefu ya Mbeya, hatakubali kupoteza kwenye uwanja wao.

Akizungumzia mchezo huo, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru, alisema wamejipanga kuvunja rekodi iliyowekwa na Azam kwa wao kuwafunga katika mchezo huo wa leo.

Kifaru alisema lengo lao ni kupata ushindi  wa pili chini ya Barnabas, baada ya kuifunga bao 1-0 Namungo katika muendelezo wa ligi hiyo.

Alisema  wamefanya maandalizi ya uhakika kuhakiksha mpinzani wao hatoki na pointi katika uwanja wao wa nyumbani wa Jamhuri.

“Tunajua Azam hawajapoteza mpaka sasa, lakini sisi tutashinda na kuvunja mwiko hasa ukizingatia kwamba tutakuwa nyumbani, mashabiki wajitokeze kwa wingi, kutuunga mkono tuweze kufanya vizuri katika mchezo huo” alisema Kifaru.

Mchezo mwingi wa ligi hiyo utakuwa kati ya  Tanzania Prisons  na Dodoma Jiji utakaochezwa kwenye kwenye Uwanja wa Samora, mjini Iringa.

Tanzania Prisons wataingia dimbani baada ya kufunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, mjini Sumbawanga.

Dodoma Jiji watakuwa na kumbukumbu ya kutoka suluhu na Kagera Sugar katika mchezo uliochezwa kwenye kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

HUJUMA NZITO YANGA

NA WINFRIDA MTOI UONGOZI wa Yanga upo katika harakati za kuhamishia mechi zao zilizobaki...

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul 'Ben Pol' ameshukuru mashabiki kwa...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -