Tuesday, October 20, 2020

MTIBWA WAITEGA SIMBA NGAO YA JAMII

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NA WINFRIDA MTOI


 

KOCHA Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema watakwenda jijini Mwanza wakiwa wameiandalia Simba dozi katika mechi yao ya Ngao ya Jamii itakayochezwa Agosti 18, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini humo.

Akizungumza na BINGWA jana, Katwila alisema hawana haraka ya kwenda jijini humo kwani hata kama wapinzani wao watatangulia mapema hawatawapa presha kwa sababu wanajiamini.

Aidha, alisema maandalizi ya mchezo huo kwa upande wao yamekamalika kwa asilimia kubwa na wanachofanya sasa ni mazoezi ya kawaida kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara.

“Sisi tupo jijini Dar es Salaam tunakabiliwa na mechi ya kirafiki dhidi ya KMC kesho (leo), ila tunatarajia kurudi mkoani Morogoro, hatuna haraka ya kwenda Mwanza tutaenda siku mbili kabla ya mechi,” alisema Katwila.

Hata hivyo, Katwila alisisitiza kwamba wanaupa uzito mchezo huo kwa sababu wanahitaji ushindi na pia hawaihofii Simba kwani ni timu ya kawaida kama zilivyo nyingine zinazoshiriki Ligi Kuu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -