Tuesday, October 27, 2020

Mtibwa waivamia Yanga kimya kimya

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA ZAINAB IDDY

KIKOSI cha wakatamiwa wa Mtibwa Sugar ni kama kimeivamia Yanga kimya kimya, baada ya kuamua kuingia jijini Dar es Salaam usiku wa Ijumaa iliyopita na kwenda kujichimbia katika Hoteli ya Itumbi, iliyopo Magomeni.

Kikosi hicho, kinachonolewa na kocha Salum Mayanga, jana jioni kilifanya mazoezi yake katika Shule ya Msingi Makurumla, kabla ya leo kuhamia Uwanja wa Bora.

Akizungumza na BINGWA, Ofisa Habari wa kikosi hicho, Thobias Kifaru, alisema timu hiyo ipo Dar es Salaam tangu Ijumaa na ilikwenda Mabatini kucheza na JKT Ruvu na kisha kurejea kambini kwao.

“Kikosi kipo katika Hoteli ya Itumbi ambako kitakaa kuusubiri mchezo wao na Yanga Jumatano ijayo, mipango yetu ni kuona tunashinda mechi hiyo.

“Msimu uliopita tulipoteza mechi zetu zote za ugenini na nyumbani dhidi ya Yanga, hivyo ligi hii hatupo tayari kufungwa tena, kwani tumejipanga kuhakikisha tunapata pointi tatu muhimu kutoka kwao,” alisema Kifaru.

Mtibwa itakutana na Yanga Oktoba 12, mwaka huu, katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakaochezwa jijini Dar es Salaam, huku Wakatamiwa hao wakiwa na kumbukumbu ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 mzunguko wa kwanza, kabla ya kuchapwa tena 1-0 mechi za lala salama katika ligi ya msimu uliopita.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -