Wednesday, October 28, 2020

MTIBWA WAJIGAMBA KUZIMA NGEBE ZA MBAO

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA WINFRIDA MTOI

KOCHA mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema wamejipanga  kuchukua pointi tatu kwa Mbao katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Oktoba 21, mwaka huu, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza  ili waweze kurejea kileleni.

Mtibwa Sugar ilishushwa kileleni na Azam baada ya kuifunga mabao 2-0 Coastal Union katika mchezo uliochezwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na BINGWA jana, Katwila alisema wanafahamu timu wanayokutana nayo ni ngumu lakini atahakikisha wanapambana nayo licha ya kwamba watakuwa ugenini.

Katwila alisema wapinzani wao wasitarajie mteremko katika mchezo huo kwa kujivunia watakuwa nyumbani, kwani msimu huu wamepania kufanya vizuri.

“Maandalizi yetu ni kushinda mchezo wetu, tulikuwa kileleni tumeshuka hadi nafasi ya pili baada ya kutoka sare na KMC, tunajua tukishinda Oktoba 21 tunarudi katika nafasi yetu,” alisema Katwila.

Mbao wanashika nafasi ya saba katika msimamo wa ligi hiyo kutokana na pointi 14 baada ya kucheza michezo tisa, ikishinda minne, sare mbili na kupoteza mitatu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -