Friday, October 30, 2020

Mtibwa yaizibua masikio Kagera

Must Read

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya...

NA SALMA MPELI

BAADA ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kutoka kwa Mtibwa Sugar, Kocha Msaidizi wa Kagera, Ally Jangalu, amesema wanahitaji kujitathmini upya.

Matokeo hayo ni kama yameizibua masikio Kagera Sugar,  waliopoteza  mchezo huo juzi kwenye Uwanja wa Manungu, mkoani Morogoro.

Akizungumza na BINGWA jana, Jangalu alisema baada ya kipigo hicho, wanakwenda kujitathimini ili kujua upungufu wa kikosi chao kabla ya kukutana na African Lyon Septemba 25, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Uhuru jijini, Dar es Salaam.

Jangalu alisema walishindwa kuibuka na ushindi kutokana na wachezaji wao kushindwa kutumia nafasi walizozipata katika kufunga mabao.

“Soka ni mchezo wa makosa, ukishindwa kutumia nafasi, basi mpinzani wako atakuzidi na kuitumia ili kupata matokeo mazuri.

“Tumepoteza mchezo, lakini wachezaji wetu kushindwa kutumia nafasi walizopata kumesababisha wapinzani wetu kuibuka na ushindi, kubwa tunakwenda kujipanga kwa mchezo unaofuata,” alisema Jangalu.

Kagera  wanashika nafasi ya tisa kutokana na  pointi sita, baada ya kucheza michezo mitano, huku Simba wakiongoza kwa pointi 13.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Hamilton avunja rekodi Ureno

LISBON, Ureno STAA wa mbio za magari Lewis Hamilton, amevunja rekodi ya Valtteri...

Ronaldinho naye ana Corona

RIO, Brazil MKONGWE wa Brazil, Ronaldinho, amethibitishwa ana virusi vya corona. Ronaldinho aliandika ujumbe kupitia ukurasa wake wa...

Sterling amlilia kinda wao Man City

MANCHESTER, England WINGA wa Manchester City, Raheem Sterling, ameandika ujumbe wa majonzi baada ya kinda wa zamani wa timu...

Afua Suleiman afunguka ‘Utalijua Jiji’ ilivyompa ustaa mjini

NA JEREMIA ERNEST JINA alilopewa na wazazi wake ni Afua Suleiman na hata alipojitupa kwenye ulimwengu wa muziki wa...

Keche: Kundi maarufu Ghana linalowatamani Diamond, Kiba, Harmonize

JIACHIE na Staa Wako, wiki hii tumetua mpaka Accra, Ghana kwa kundi maarufu la muziki nchini humo, Keche linofanya vizuri na ngoma...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -