Friday, November 27, 2020

MTOTO CHANZO CHA WIZ KHALIFA NA AMBER ROSE KUNG’ANG’ANIANA

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

LOS ANGELES, Marekani

MOJA kati ya habari zinazopendwa na kufuatiliwa na mashabiki wengi wa burudani, ni ile inayohusu uhusiano wa kimapenzi kati ya mwanamuziki, Wiz Khalifa na mwanamitindo, Amber Rose.

Mapenzi ya mastaa hao yamekuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki wao, hasa kutokana na ukweli kwamba vitendo vyao vya ‘kisela’ vimekuwa vikifanana mno.

Kwa mara ya kwanza, taarifa za wawili hao kuwa na uhusiano wa kimapenzi zilianza kuteka vichwa vya habari za burudani mwaka 2011.

Hiyo ilikuwa ni miezi michache baada ya Amber kuachana na mwanamuziki wa hip hop, Kanye West.

Baada ya kuwa kwenye uhusiano uliodumu kwa miaka miwili, Wiz na Rose walioana mwaka 2013 na baadaye walibahatika kupata mtoto wa kiume aitwaye Sebastian. Hata hivyo, ndoa yao ya miaka mitatu ilivunjika mwaka 2016.

Kuanzia hapo wawili hao walitengana na kila mmoja aliishi kivyake.

“Nahisi kama tulikimbilia kuoana kwa sababu tulipendana sana, hatukua na furaha katika ndoa yetu,” alisema Amber ambaye pia aliwahi kutoka kimapenzi na rapa Kanye West na kuongeza:

“Nafikiri kama tungekuwa wapenzi kwa kipindi kirefu, basi tungeweza kudumu kwenye ndoa.”

Hata hivyo, uhusiano wao umeendelea kuwa hai kwa kiasi fulani kutokana na mtoto wao Sebastian.

Mara kadhaa Wiz amekuwa akimtembelea Rose kwa lengo la kumuona mtoto wake huyo, jambo ambalo limekuwa likiibua madai kuwa bado wawili hao wanaendeleza uhusiano wao.

Katika moja ya vipengele vya talaka yao, wawili hao walikubaliana kushirikiana katika malezi ya ‘dogo’ Sebastian ambapo Wiz amekuwa akitoa Dola za Marekani milioni 14,800 (zaidi ya Sh milioni 30 za Tanzania) kwa mwezi.

Akizungumzia uhusiano uliopo kati ya kuvunjika kwa uhusiano wake na Amber na mtoto wake alisema: “Nilisikitika tulipoachana, lakini sikukata tamaa. Sijawahi kukatishwa tamaa katika maisha yangu. Nilisikitika kwa sababu ilimhusu mtoto wangu. Iliniuma kwa sababu lengo langu lilikuwa ni kumlea mtoto wangu kwa namna niliyoitaka. Kwa sasa nimeshazoea (kuishi bila Amber).”

Juzi wawili hao walikuwa pamoja kwenye hafla ya utoaji Tuzo za Grammy na hilo limeibua shaka kuwa huenda wanaendelea kujiachia kimya kimya.

Kitendo cha Wiz na Amber kupigana mabusu hadharani wakati wa hafla hiyo, kimeibua maswali mengi na kuna kila dalili za mastaa hao kufufua mapenzi yao.

Hiyo imekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu mlimbwende Amber alipotemana na aliyekuwa mpenzi wake, Val Chmerkovskiy.

Uhusiano wa Amber na dansa huyo umevunjika ikiwa ni baada ya kudumu kwa kipindi kifupi cha miezi mitano tu.

Kwa upande wake, baada ya kutemana na Amber, Wiz alitua kwenye penzi la mwanadada Natalie Nunn ambaye ni mtangazaji wa vipindi vya televisheni.

Baadaye alitemana naye na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi na mrembo Draya Michele. Pia, Wiz amewahi kupumzika kimahaba na walimbwende Indya Marie na Deelishis.

Kuna kipindi Wiz alitajwa kuwa na uhusiano na straa wa pop, Selena Gomez, ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Justin Bieber.

Jambo hilo lilionekana kumchoma Amber na ndipo chanzo kimoja cha habari kilipodai: “Selena anacheza na moto, si tu atamtibua Amber, lakini pia Wiz ni msumbufu.”

Chanzo hicho hakikuweza wazi ni kwa namna gani Amber angechanganyikiwa kusikia mume wake huyo wa zamani anatoka na Selena, hasa kwa kipindi hicho alichokuwa na staa wa mpira wa kikapu, Terrence Ross.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -