Sunday, November 29, 2020

MTV BASE AFRICA WAPO SAHIHI, BEN POL USICHUKIE

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA CHRISTOPHER MSEKENA,

WIKI hii kituo cha runinga cha MTV Base Africa kiliweka haradhani orodha ya majina ya wasanii wa kutazamwa zaidi mwaka huu. Miongoni mwa majina hayo kulikuwa na mastaa kutoka Bongo Fleva, Ray Vanny na Ben Pol.

Kwa upande wa Ray Vanny, hakukuwa na tatizo kutokana na uchanga wake kwenye muziki, kwa Ben Pol hali ilikuwa tofauti, kwani wengi waliona wazi kituo hicho cha runinga kimemshushia hadhi staa huyo wa singo ya Phone.

Hali hiyo ilitokana na ukweli kuwa, Ben Pol alitoa wimbo wake wa kwanza, Nikikupata miaka 7 iliyopita, sawa kabisa na Diamond Platnumz, aliyetoboa kwa Mbagala, Wizkid aliyepata ustaa kupitia singo ya Holla at Your Boy, hali kadhalika Davido aliyefahamika kupitia Dami Duro.

Kwa hiyo Ben Pol ana umri sawa na Davido, Diamond Platnumz na Wizkid kwa kipimo cha miaka yao kwenye tasnia ya muziki. Na leo unapomfananisha na Ray Vanny ambaye ana singo mbili tu unakuwa humtendei haki.

Kuna tatizo?

Ben Pol mpaka sasa ana ‘hit song’ zaidi ya kumi kama vile Samboira, Number One Fan, Maneno, Jikubali, Unanichora, Sophia, Pete, Ningefanyaje, Moyo Mashine na Phone.

Ukiyatazama mafanikio ya mkali huyu wa RnB utagundua yanakuja taratibu, tofauti na yanavyoonekana dhahiri kwa Diamond Platnumz, Davido na Wizkid.

Ben Pol, hivi sasa huwezi kumfananisha na Diamond Platnumz, ambaye ni staa mkubwa Afrika, pia mafanikio makubwa aliyonayo Davido huwezi kuyalinganisha na aliyonayo Ben Pol, hali kadhalika Ben Pol haingizi mguu kwa Wizkid, japokuwa wote walianza muziki mwaka mmoja.

Nafasi ya Ben Pol Afrika

Licha ya kuwa na nyimbo nyingi zilizofanya vizuri, Ben Pol ameanza kuonekana zaidi kwenye soko la muziki wa Afrika kupitia singo zake mbili za Moyo Mashine na Phone, aliyomshirikisha Mr Eazi kutoka Ghana.

Mpaka sasa Ben Pol anamiliki albamu moja ya Maboma, kitu ambacho kinamuweka mbali kabisa na levo walizonazo kina Wizkid, Davido na Diamond Platnumz, ambao wana albamu zaidi ya moja na wamekuwa wakitoa hyimbo zinazo-hit Afrika nzima.

Ommy Dimpoz…

Moja ya vigezo vya ukubwa wa mwanamuziki siyo idadi ya miaka aliyonayo kwenye tasnia, bali ukubwa wa msanii hupimwa kwa kazi zake, hasa wingi wa albamu.

Unaweza kuwa na miaka mingi kwenye muziki, lakini ukaonekana ni msanii mpya kwa sababu huna vigezo vya kuthibitisha ukubwa wako, na moja ya vithibitisho ni wingi wa albamu na siyo idadi ya singo.

Hali hii iliwahi kumkuta Ommy Dimpoz, ambaye ni staa wa singo kali kama Nai Nai, Ndagushima, Baadaye, Tupogo na Me And You, pale alipowekwa kwenye kipengele cha wasanii chipukizi katika tuzo za Afrimma zilizotolewa Dallas, Marekani mwaka 2015.

Sasa Ommy Dimpoz na ustaa wake wote ule aliwekwa kwenye kipengele cha ‘Best New Comer’ na chipukizi wengine wa Afrika, iweje leo tupinge uwepo wa Ben Pol kwenye orodha ya wasanii wa kutazamwa mwaka huu?

MTV Base Africa wamekosea?

Hawajakosea, kwa sababu ni kweli wameanza kumuona Ben Pol, baada ya kufanya uwekezaji kwenye muziki wake kupitia nyimbo kama Moyo Mashine na Phone, licha ya huko nyuma Watanzania walimfahamu kwa kazi zake nyingi mpaka wakampachika jina la Mfalme wa RnB.

Ben Pol chukua hii

Hii ni nafasi nzuri kwako kuonyesha kuwa wewe ni zaidi ya wasanii wapya waliowekwa pamoja nawe kwenye orodha ile.

Tayari umejitengenezea nafasi kwenye soko la muziki wa Afrika, tunahitaji kazi zaidi ya Moyo Mashine na Phone na zaidi usisahau albamu kwa sababu ukubwa wa msanii makini hupimwa kutokana na idadi ya albamu.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -