Saturday, November 28, 2020

MUME ANAPONASA KWA ‘HOUSE GIRL’

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

NA MICHAEL MAURUS

KARIBUNI ndugu wasomaji wa gazeti hili katika safu hii ambayo inawajia kila Jumanne ikilenga kujuzana hili au lile, kuhusiana na suala zima la uhusiano wa kimapenzi baina ya wawili waliopendana.

Awali ya yote, nitoe pongezi za dhati kwa wale wote ambao wamekuwa wakichangia katika mada zangu kwa kuuliza au kutoa shuhuda mbalimbali.

Baada ya wiki kadhaa zilizopita kujadili jinsi ya kubaini penzi la dhati, leo tuhamie katika mambo yanayoweza kuwa sumu kwa uhusiano wa wawili waliopendana na hatimaye kuwatenganisha.

Yapo mengi, lakini kwa leo tuone jinsi wasaidizi wa majumbani wanavyohatarisha uhusiano baina ya wapenzi au hata wanandoa.

Mara nyingi wafanyakazi wa ndani wamekuwa wakijikuta wakianzisha uhusiano wa kimapenzi na mabosi wao kutokana na sababu mbalimbali.

Wapo wasichana wa kazi ambao walijikuta wakiwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na baba mwenye nyumba au mvulana wa kazi kuangukia kwa mama mwenye nyumba.

Moja ya sababu ya baba mwenye nyumba kuanzisha uhusiano wa kingono au kimapenzi kwa ujumla na msichana wake wa kazi, ni kujisahau au ulimbukeni wa baadhi ya wake zao katika kutekeleza majukumu yao ndani za uhusiano au ndoa zao, hivyo kuwafanya waume zao ‘kupitiwa na shetani’ na kujihusisha kimapenzi na wasichana wao wa kazi (house girl).

Katika hilo, wake wamekuwa wakiwapa nafasi wasichana wao kuwa karibuni na waume zao, mathalani kwa kuwatengea chakula, maji ya kuoga na kazi nyingine kama hizo.

Unaweza kukuta mke akitumia muda mwingi kujiangalia yeye binafsi akisahau kuwa ni wajibu wake kuhakikisha mume wake anakula nini, chakula kinahifadhiwa wapi, anavaa nini na mengine kama hayo na kumwachia kazi hiyo msichana wake wa kazi.

Mwisho wa siku, mume anajikuta akiwa karibu zaidi na msichana wake wa kazi na matokeo yake, hujikuta akizidiwa na kufanya kile ambacho hakikutarajiwa.

Kuna rafiki yangu aliwahi kunisimulia kuwa aliachana na mke wake kutokana na penzi la msichana wake wa ndani ambaye alikuwa akimjali mno kuliko alivyokuwa akifanya mke wake huyo.

Jamaa alisema kutokana na jinsi msichana wao huyo wa ndani alivyokuwa akimhudumia yeye pamoja na watoto wake, wakati mke wake akiwa aidha anafanya shughuli zake binafsi au amelala, aliamua kulipa fadhila kwa kuwa naye karibu zaidi.

“Siku moja nilipowasili nyumbani nikitokea kazini, nilimkuta binti yule akiwa ananisubiri ili anitengee chakula na maji ya kuoga kama kawaida yake. Nilimwita na kuanza kuzungumza naye. Nilimtaka amuage mke wangu kuwa anakwenda kwa dada yake Kibaha kusalimu na atarudi kesho yake. Nilimwambia kuwa akishatoka nyumbani anipigie simu nimweleze anikute wapi,” alisimulia jamaa yule.

Alisema siku iliyofuata msichana yule alifanya kama alivyomfundisha. Alimpitia sehemu aliyomwelekeza amkute na kwenda naye nje ya jiji ambako alichukua chumba katika moja ya nyumba ya wageni na kulala huko na binti yule.

“Yule binti alinieleza mambo mengi mno anayofanya mke wangu pale nyumbani ambayo sikuwa nikiyafahamu kabla. Kwa mfano, kitendo cha kumwachia msichana wa watu kufua hata nguo zake za ndani,” alisimulia na kuongeza:

“Kutokana na maelezo ya binti yule, roho iliniuma mno, niliona ni vema nikaishi na mtu anayejua ninatakiwa kula nini, kuvaa nini na kuoga nini. Kikubwa zaidi, nilijisemea moyoni nitastahili kuishi na mke anayewajali watoto wangu, ambaye kila siku atakuwa akijua wajibu wake katika kuifanya nyumba yake kuwa yenye amani, furaha na upendo wa hali ya juu.”

Alisema ilipofika asubuhi, alikwenda moja kwa moja nyumbani kwake na kumfukuza yule mke wake ambaye hata hivyo, hakutaka kuondoka. Aliamua kumwachia vyumba viwili walivyokuwa wamepanga na kuwachukua watoto wake na baadhi ya vitu vinavyobebeka na kwenda kuishi kwa rafiki yake wakati akitafuta vyumba vya kuishi pamoja na watoto wake na ‘mama yao mpya’ ambaye awali alikuwa kama msichana wa kazi.

“Ndio huyu shemeji yako wa sasa niliyezaa naye mtoto mmoja, ambaye ananipenda sana, nami ninampenda pia. Anawajali watoto wangu nao pia wanampenda na wala hawana hamu na mama yao ambaye nasikia aliolewa na mwanamume mwingine akaachika kwa sasa yupo yupo tu,” alimalizia kusimulia.

Ndugu msomaji, hebu niurudishe mpira kwenu juu ya mada hii kabla ya wiki ijayo kuihitimisha. Je, nini kinachangia mume kujikuta ‘akioza’ kwa msichana wake wa kazi, ni uroho au? Usikose toleo la Jumamosi

 

Tuma maoni yako kupitia namba 0713556022 au anuani pepe: michietz@yahoo.com

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -