Wednesday, October 21, 2020

MURRAY: VERDASCO KUVUNJA SHERIA SI POA MZEE!

Must Read

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu...

NEW YORK, Marekani


KITENDO cha kocha wa Fernando Verdasco, kuingilia pambano la tenisi la raundi ya pili michuano ya US Open lililochezwa mapema wiki hii, dhidi ya Andy Murray, kimetafsiriwa kuwa ni uvunjifu wa kanuni na mkali huyo kutoka England.

Murray alisema kwamba, mpinzani wake na timu yake kwa ujumla walishindwa kuheshimu kanuni za waandaaji wa mashindano hayo yanayoendelea nchini Marekani.

Kutokana na hali ya hewa ya joto kali inayolikabili Jiji la New York wiki hii, waandaaji hao waliunda sheria mpya ya kuruhusu mapumziko ya dakika 10 kati ya seti ya tatu na nne, katika mapambano ya wanaume.

Katika muda huo wa mapumziko, wachezaji hawaruhusiwi kuzungumza na makocha wao, kitu ambacho Murray alisema alimwona Verdasco akikifanya alipomaliza kujimwagia maji baridi.

Mara baada ya kushuhudia jambo hilo likifanyika, Murray alikasirika na kumfuata mwamuzi, Nico Helwerth, kumweleza kila kitu mara tu waliporudi dimbani.

“Ilinibidi niwaambie kwa sababu niliona hawazijui sheria,” alisema Murray ambaye alipoteza pambano lake hilo kwa seti 7-5, 2-6, 6-4 na 6-4.

“Pia niliwauliza waamuzi kwanini wanaruhusu mambo kama haya kutokea ikiwa wanazifahamu sheria ndio wakashtuka. Kwa kweli itabidi wakati mwingine wawe makini maana hii ni moja ya michuano mikubwa,” aliongeza Murray.

Hata hivyo, Verdasco alikanusha kwamba hakuvunja sheria, akidai kwamba alizungumza na mchezaji mwingine, Marcos Baghdatis, pamoja na kocha wa Baghdatis.

“Siwezi kusema Murray amesema uongo, lakini sikuzungumza na kocha wangu au mchezaji wa timu yangu. Naifahamu sheria vizuri sana na sitaki niwe mmoja wa wanaoivunja,” alisema Verdasco.

Clarke, Molard wafanya

kweli ‘Vuelta a Espana’

MADRID, Hispania

NYOTA wa baiskeli kutoka Australia, Simon Clarke na Mfaransa Rudy Molard, wameendelea kutisha katika mbio za baiskeli zinazofanyika nchini Hispania (Vuelta a Espana).

Clarke aliibuka mshindi katika raundi hiyo ya tano ya mbio hizo, huku Molard akipambana vilivyo na kuchukua uongozi wa orodha ya madereva bora, iliyokuwa ikishikiliwa na Mwingereza, Michal Kwiatkowski.

Clarke aliibuka mshindi mwishoni mwa mbio hizo za kilomita 188.7, kuanzia Granada hadi Roquetas de Mar, akiwapiku Mholanzi, Bauke Mollema na Alessandro De Marchi wa Italia.

Licha ya Molard kumaliza katika kundi la pili, akiachwa kwa sekunde nane, lakini aliweza kuchukua nafasi ya Kwiatkowski ambaye alizidiwa kasi mwishoni mwa mbio kwa zaidi ya dakika tano.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Director Kenny: Harmonize alinipeleka WCB nikafanya video ya Lavalava

MWONGOZAJI bora wa video nchini, Kenned Sanga a.k.a Derector Kenny kutoka Zoom Extra, ametua   hapa Jiachie na...

Rogers mwanamuziki anayevutiwa na Marijani

NA JEREMIA ERNEST BONGO Star Search (BSS), ni shindano lililofanikiwa kuibua vipaji vingi vya wanamuziki wa Tanzania ambao miongoni...

Ihefu, Azam patachimbika Sokoine, Katwila ndani

NA ASHA KIGUNDULATIMU ya Ihefu inatarajia kushuka uwanjani kucheza na Azam ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara  (VPL), utakaochezwa leo...

Mugalu atema cheche Simba

NA ASHA KIGUNDULA MSHAMBULIAJI wa Simba, Chris Mugalu, amesema wanakwenda mkoani Rukwa kupambana na kupata ushindi katika mchezo wao...

Malale aitisha Yanga

NA ZAINAB IDDY KOCHA Mkuu wa timu ya Polisi Tanzania, Malale Hamsini, amezisikia sifa za kocha mpya wa Yanga,...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -