Wednesday, November 25, 2020

MUUE LEICESTER UMPE LEVERKUSEN YA CHICHARITO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

KUANZIA Februari hadi kufikia Mei, timu mbalimbali zitakutana na mkusanyiko wa mechi za ligi na zile za kuwania makombe kama Uefa, Europa, Copa Italia, FA, EFL na mengineyo.

Wikiendi hii baadhi ya ligi zitasimamishwa ili kupisha mechi za kuwania makombe hayo na mzee wa kubeti leo naendelea kukupa dondoo za kuusuka mkeka wako. Nasemaje, usichane mkeka.

 

Wolverhampton vs Chelsea

Wolves waliinyuka Liverpool bao 2-0, kabla ya kuichapa Barnsley, lakini baada ya hapo kuna bundi aliwapitia na mechi tatu zimefululiza bila kuuonja ushindi.

Nafasi waliyopo kwenye ligi ya Championship (18) si ya kuridhisha na wanawakaribisha vinara wa Premier League ambao si wepesi kuangushwa msimu huu. Kuna uwezekano wa mchezo huu kuwa na mabao mengi, hasa kipindi cha pili. Mpe Chelsea bila kusita.

Utabiri: Wolves 0-3 Chelsea

 

Marseille vs Rennes

Miamba ya Ufaransa, Marseille ni wazi wanahitaji kucheza Uefa msimu ujao lakini wataingiaje? Ni lazima washinde mechi kama hizi dhidi ya timu dhaifu.

Wikiendi iliyopita walibugizwa 3-2 lakini kesho sioni uwezekano wa Rennes  kuiangusha Marseille nyumbani kwake. Sehemu mahususi kwa wao msimu huu.

Utabiri: Marseille 2-0 Rennes

 

Augsburg vs Bayer Leverkusen

Wenyeji bado hawajakaa sawa. Katika mchezo wa wikiendi iliyopita walifungwa, ni siku waliyotarajiwa kufanya vizuri zaidi ili angalau wawe na mechi tatu za ushindi ambazo zingewawezesha kupanda hadi nafasi 10 za juu.

Mchezo wao wa wikiendi hii dhidi ya Leverkusen ya straika Javier Hernandez ‘Chicharito’, ni mtihani mzito kwani kikosi hicho kitataka kutumia faida ya hali halisi inayoendelea kwa Augusburg.

Utabiri: Augsburg 1-2 Leverkusen

 

Sporting Gijon vs Atletico Madrid

Siku chache zijazo Atletico watacheza mchezo wao wa kwanza wa 16 bora Uefa dhidi ya Leverkusen, huku pia wakikabiliwa na jukumu la kurudisha matumaini yao ya kunyakua ubingwa wa La Liga.

Atletico hii ambayo haitakuwa na beki wake, Diego Godin, itapata shida tena wikiendi hii kama mechi mbili zilizopita waliporuhusu mabao yaliyokuwa na uwezo wa kuzuilika. Bila Godin, Atletico ni timu nyepesi kufungika hivyo kuifanya mechi hiyo kuwa na uwezekano wa pande zote mbili kupata bao.

Utabiri: Gijon 2-2 Atletico

 

Millwall vs Leicester City

Mabingwa watetezi wa Premier League wamekuwa mabingwa walegevu! Na huenda machungu yakazidi kabisa kadiri siku zinavyozidi kwenda.

Wikiendi hii kwenye mechi za Kombe la FA watavaana na Millwall ugenini. Baada ya kuichapa Derby County wiki iliyopita na kushindwa kuendeleza ushindi dhidi ya Swansea, mtihani mwingine utakuwa ni dhidi ya Millwall, Claudio Ranieri, bila shaka atashawishika kufanya mabadiliko ya kikosi chake. Hapo kuna mawili, kulia au kucheka.

Utabiri: Millwall 2-0 Leicester

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -