Saturday, November 28, 2020

MWACHENI MARADONA AMLILIE FIDEL CASTRO

Must Read

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali...

HAVANA, Cuba

NI siku chache zimepita tangu mwanasiasa mashuhuri ulimwenguni, Fidel Castro, alipoiaga dunia.

Rais huyo wa zamani wa Cuba alifariki Novemba 25 na kuacha simanzi kubwa si tu nchini humo bali kwenye medani ya siasa kwa ujumla.

“Mkuu wa Majeshi wa Mapinduzi ya Cuba alifariki saa 22:29 (4 usiku),” alisema Raul na kuongeza: “Hasta la Victoria siempre (ushindi daima)!

Kutokana na uzito wa tukio hilo, Serikali ya Cuba ilitangaza kuwa wananchi watapata mapumziko yatakayofikia tamati Desemba 4 na taarifa ziliongeza kuwa mwili wa rais huyo utapumzishwa jijini Santiago.

Taarifa za kifo cha Castro zilitolewa  na kaka yake ambaye ndiye rais wa sasa wa Cuba, Raul, kupitia kituo kimoja cha runinga cha nchini humo.

Hata hivyo, si wengi wanaojua kuwa Castro alikuwa na uhusiano mkubwa na mchezo wa soka. Ni wachache mno wanaojua kuwa hata Castro alikuwa shabiki wa kandada.

Kuna historia ndefu sana kati ya Castro na aliyekuwa mpachikaji mabao wa klabu ya Napoli na timu ya Taifa ya Argentina, Diego Maradona.

Uswahiba wa Castro na Maradona ulianza muda mrefu na ni kipindi hicho ndipo mwanasoka huyo alipokuwa akitamba na klabu yake ya Napoli.

Wengi wanaamini kuwa Maradona ana deni kubwa kwa Castro na huenda akawa ndiye binadamu atakayemkumbuka zaidi mwanasiasa huyo.

Tukirudi kwenye historia ya urafiki kati ya Castro na Maradona, wawili hao walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1986.

Kipindi hicho, Maradona alikuwa ametoka kuifanyia makubwa Argentina kwani aliiongoza kunyakua taji la fainali za Kombe la Dunia.

Maradona alikwenda hadi ikulu kumtembelea Castro na kuanzia hapo akawa anaingia Cuba kila alipojisikia kufanya hivyo.

Hata hivyo, Mardona alipostaafu ndipo urafiki wao ulipokolea zaidi hasa baada ya mwanasoka huyo kuingia kwenye utumizi wa dawa za kulevya.

Maradona alikuwa mtumiaji mzuri wa dawa za kulevya aina ya Cocaine na kuna kipindi afya yake ilikuwa mbaya, hivyo alihitaji msaada wa madaktari bingwa.

Kutokana na ubora wa huduma ya afya iliyopo Cuba, Castro alijitolea kumpa nafasi Maradona ya kutibiwa nchini humo.

Baada ya kutua Cuba na kupata huduma ya kiafya, Maradona alipona kabisa na kuanzia hapo alitangaza kuachana na dawa za kulevya.

Akizungumzia hilo baada ya kifo cha Castro, Maradona alikiambia kituo cha televisheni cha TyC Sports: “Alikuwa kama baba kwangu. Lazima nitakwenda kumuaga rafiki yangu. Alinifungulia milango ya kuingia Cuba pale Argentina iliponipotezea.”

Ni wazi kabisa kuwa mashabiki wa soka wanatakiwa kuhuzunika kwa kifo cha Castro kwani huenda bila yeye wangemkosa kipenzi chao Maradona.

Mbali na soka, ulimwengu wa siasa utaendelea kumkumbuka Castro hasa kutokana na uimara wake katika kusimamia misingi ya Kiujamaa.

Itakumbukwa kuwa Castro ndiye aliyeupindua utawala wa Batista na kujenga siasa za Ujamaa mwaka 1959 na katika kufanikisha hilo, alipata msaada mkubwa kutoka kwa mwanaharakati Che Guevara.

Yajue haya kuhusu Castro

Castro alikuwa mmoja kati ya wanasiasa matajiri. Miaka 10 iliyopita, jarida la Forbes lilimtaja Castro kuwa na utajiri wa Dola za Marekani milioni 900.

Lakini pia, Castro alikuwa na ulinzi mkubwa hasa kutokana na kukumbana na majaribio ya kuuawa mara kadhaa. Inaaminika kuwa hata wananchi wa Cuba hawakujua rais wao huyo alikuwa akiishi wapi.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

BEN POL AJA NA HIYO NDIO MBAYA

Na Mwandishi Wetu MSANII nguli wa muziki wa R&B na Bongo Fleva Benham Paul...

ZILE NI SALAM TU

NA MWANDISHI WETU KIPIGO cha mabao 7-0 walichokitoa Simba juzi kwa Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania...

DEWJI: CHAMA NI SIMBA HADI 2022

Kiungo huyo raia wa Zambia, aliyetoa mchangomkubwakwaSimbakufikisharobo fainaliyaLigiyaMabingwaAfrikamsimuwa 2018/19, ikiwamo kutwaa ubingwa wa LigiKuuTanzaniaBarakwa misimumitatu mfululizo, awali ilidaiwa alikuwa yupo katika hatuayamwishoyakujiunganaYanga.

Sven aruka kihunzi

NA ASHA KIGUNDULA KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck, ameruka kihunzi na kuwaachia msala nyota wake, Clatous Chama na...

Sarpong ‘aua’ shabiki Simba

Na MWANDISHI WETU, MWANZA BAO la dakika ya 29 lililofungwa na Michael Sarpong wa Yanga juzi, limesababisha kifo cha...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -