Monday, October 26, 2020

MWAKA 2017 UWE MWOKOZI WA BONGO MOVIE

Must Read

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa...

NA HASSAN DAUDI

MWENYEZI Mungu pekee ndiye anayepaswa kushukuriwa kwa kutuwezesha kutuvusha katika mwaka mwingine wa 2017.

Pamoja na changamoto nyingine za kimaisha, kuwa miongoni mwa watu waliofanikiwa kuona mwaka mpya ni jambo la heri.

Lakini  tukianza kukimbizana na mipango yetu ya mwaka huu mpya, bado tunapaswa kuendelea kutathmini pia miezi 12 iliyopita.

Nikiri wazi kuwa mwaka 2016 ulikuwa wa mafanikio makubwa kwa wanamuziki wa Bongo Fleva. Hakika waliweka juhudi kubwa kwenye kazi zao na hatimaye matunda yake yalionekana.

Ikiongozwa na mastaa Nasib Abdul ‘Diamond Platinum’ na swahiba wake mkubwa,  Ali Kiba, Bongo Fleva ilivuna tuzo nyingi hasa zile zinazoandaliwa nje ya mipaka ya nchi yetu.

Kwa mwaka 2016, Tanzania iliwaka vilivyo kwenye tuzo za muziki za nje ya nchi.

Kwa upande mwingine, tasnia ya filamu ‘Bongo Movie’ iliendelea kujikongoja mbele ya wenzao wa Bongo Fleva.

Mdororo wa soko la filamu za hapa nyumbani uliendelea kuwa kaulimbiu ya mkashabiki na waigizaji wa tasnia hiyo.

Kwa utafiti mdogo, utagundua kuwa kumekuwa na matatizo mengi mno kwenye tasnia ya filamu, hivyo kuangukia pua mwaka jana isingeweza kuwa tukio la kushangaza sana.

Hata hivyo, Waswahili wanasema kujikwaa si kuanguka. Kama wasanii wa Bongo Movie watajipanga, huenda mwaka 2017 ukawa wao na kuwafunika wenzao wa Bongo Fleva.

Natamani kuona mwaka 2017 ukija na mapinduzi makubwa ya tasnia ya filamu hapa nchini kama walivyofanya Bongo Fleva miezi 12 iliyopita.

Hilo litawezekana kama wasanii wa Bongo Movie watautumia mwaka huu kutokomeza madudu ambayo yamekuwa yakiwatesa kwa kipindi kirefu.

Simaanishi kuwa wasanii wa Bongo Fleva hawana madudu yao, ikiwamo kutegemea ‘CD’ wanapokuwa jukwaani, lakini hatua waliyofikia inatia moyo kwa kiasi fulani.

Kwanza, ni wakati wa waigizaji wetu kutambua umuhimu wa weledi kwenye kazi zao ambazo zimekuwa zikiingizia nchi pato kubwa huku zikiwa chanzo cha ajira kwa vijana wengi wa Kitanzania.

Ieleweke vizuri kuwa moja kati ya sababu ya kifo cha Bongo Movie ni kupuuzwa kwa misingi ya weledi (professionalism).

Weledi hauonekani kuwa na umuhimu mkubwa kwenye sanaa ya uigizaji. Ili uwe na sifa ya kuingia ‘Bongo Movie’, unatakiwa kuwa na kipaji tu. mengine utajifunzia huko huko.

Hatukatai kuwa kipaji ni muhimu lakini ili kukabiliana na ushindani uliopo kwenye soko la kimataifa, elimu ina nafasi yake kubwa.

Ni wasanii wangapi wa Bongo Movie wanaoweza kusimama hadharani na kuonyesha vyeti vyao vya elimu ya sanaa? Ni aibu tupu.

Kwa sampuli ya haraka, kati ya wasanii 10 utakuta ni wawili tu waliokaa darasani na kupewa elimu ya masuala ya sanaa.

Nani asiyejua kuwa kuna idadi kubwa ya wasanii wa kike ambao walipata nafasi ya kuigiza baada ya kuonekana kwenye mashindano ya urembo.

Kwa kuwa umaarufu umekuwa kigezo cha kuwa mwigizaji, kumekuwa na lundo la watangazaji wa vituo vya televisheni na redio, mapropdyuza, wanamuziki kwenye filamu zetu.

Ukiwauliza waliingiaje kwenye tasnia hiyo, watakwambia waliambiwa wana vipaji. Mambo haya ya kipuuzi hayapaswi kupewa nafasi mwaka huu.

Dunia imebadilika mno, hata sanaa ni taaluma inayohitaji watu makini na wenye uelewa wa kutosha juu ya kazi hiyo.

Hatuwezi kuifufua Bongo Movie mwaka 2017 kama kigezo cha kumpata mwigizaji wa kike kitaendelea kuwa uzuri wa sura na umbo lake, badala ya elimu aliyonayo kwenye sanaa.

Lakini pia, huenda mwaka huu Bongo Movie ikaendelea kubaki shimoni ikiwa msanii aliyeigiza ‘muvi’ mbili ana uwezo wa kuwa ‘dairekta’.

Kuna orodha ndefu ya wasanii ambao wamekuwa wakijiita madairekta huku wakiwa na uwezo mdogo wa kuifanya kazi hiyo.

Mwigizaji anaweza kuwa mwongozaji wa filamu, lakini je, anafahamu kuwa hizo ni taaluma mbili tofauti? Ana elimu ya kutosha kujibebesha jukumu hilo?

Hao ndio wanaotuzalishia kazi mbovu ambazo zimeendelea kuwakimbiza mashabiki wa filamu ambao kwa sasa wameamua kujikita kwenye filamu za mwendelezo ‘series’ kutoka Japan na Korea.

Naamini waigizaji wetu wana uwezo wa kutanua wigo wao kimataifa kama wenzao hao. Ni kujipanga tu. Sina shaka kuwa mwaka 2017 umekuja kwa ajili ya Bongo Movie. Tafadhali msiniangushe.

- Advertisement -

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

- Advertisement -

Latest News

Boni Mwaitege amkalisha Mgogo

NA VALERY KIYUNGU KUPITIA shindano la Nani Zaidi linaloendeshwa na redio Passion Fm ya...

Mzuka warudi tena kwa s2kizzy

NA CHRISTOPHER MSEKENA SIKU chache baada ya kuvamiwa na kufanyiwa uharibifu wa studio zake za Pluto Republic, prodyuza nyota...

The Yeamen waipiga ‘Shoti’

NA JEREMIA ERNEST MSANII kutoka kundi la The Yeamen, Suma Toto, amewaomba mashabiki wa Bongo Fleva kuendelea kulipa sapoti...

JB Maeba atimiza ndoto zake na Cannibal

NA CHRISTOPHER MSEKENA MSANII wa Afro Pop na Bongo Fleva anayeishi Kenya, James Tesha a.k.a JB Maeba, amesema anafurahi...

‘Certified Lover Boy’ ya Drake yaiva

TORONTO, CANADA RAPA nyota ulimwenguni, Aubrey Graham maarufu kama Drake, ametangaza habari njema ya ujio wa albamu yake ya...
- Advertisement -

More Articles Like This

- Advertisement -